Muda mfupi baada ya kutolewa kwa taarifa ya Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Said Sultan kukamatwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Klabu hiyo imetoa tamko na kueleza kuwa hakuwa mwajiriwa wa klabu hiyo.
Taarifa
iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu ya Simba, imeeleza kuwa Muharami hakuwa
mwajiriwa bali aliombwa kuwanoa makipa kwa muda wa mwezi mmoja wakati klabu
ikiendelea kutafuta kocha wa magolikipa.
Taarifa hiyo
imeongeza kuwa, haihusiki na tuhuma zinazomkabili kocha huyo na kuwataka
mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yoyote inayoweza
kuikumba klabu hiyo kutokana na kadhia iliyomkumba kocha huyo.
Taarifa ya
Muharami pamoja na watuhumiwa wengine 8 kukamatwa, zimetolewa leo na Kamishna
Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
0 Comments