Header Ads Widget

IDADI YA VIFO VYA AJALI YA GARI MANYARA YAONGEZEKA.


Idadi ya vifo vilivyosababishwa na ajali ya gari iliyotokea eneo la Pori Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imefika saba baada ya majeruhi mmoja kufariki akiwa katika Hospitali ya Dodoma. 

Ajali hiyo ilitokea jana Jumatatu Novemba 07, 2022 baada ya gari la kubeba wagonjwa kugongana uso kwa uso na gari lingine aina ya Prado. Jana, taarifa zilithibitisha vifo vya watumishi sita wa Serikali, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wakiwamo mke na mume. 

Hata hivyo, leo Jumanne Novemba 8, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara (RPC), George Katabazi amesema mtu mwingine alifariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kutolewa katika hospitali ya Kiteto. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI