Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Jakaya Kikwete ameahidi kuendelea kuisaidia Halmashauri ya Chalinze kwa kadri ya uwezo wake kama alivyokua kabla, wakati na hata baada ya kustaafu nafasi mbalimbali za Uongozi kwa kuwa Halmashauri hiyo ya Chalinze na wilaya ya Bagamoyo ndipo nyumbani kwao .
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Madiwani, Watumishi wa Umma na viongozi wengine wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze.
“Kukubali kwangu kuja kuzungumza nanyi hapa Mimi hii ndio Halmashauri yangu, nimdau wa Chalinze kwa kuzaliwa , kwaiyo sina halmashauri nyingine hata kama nikienda kuishi sehemu nyingine huko nimeenda tu kuishi lakini huku ndio kwetu na ningependa kuona kwetu kunapiga hatua kimaendeleo”_ Alisema
“Chochote ninachoweza kuchangia nitafanya kama ambavyo nimefanya kipindi chote, nilipokua Mbunge, nilipo kuwa Waziri, Rais na hata baada ya Kustaafu”.Aliongeza Rais Mstaafu Kikwete.
Aidha aliwataka Madiwani katika halmashauri zote nchini kutambua kuwa ndio wenye wajibu wa kupanga na kusimamia shughuli zote za maendeleo hivyo kuondoa dhana ya miongoni mwao kuonekana kuwa sehemu ya wanaolalamika.
“Halmashauri zimekabidhiwa shughuli zote za maendeleo baada ya Ugatuzi wa Madaraka na kwenye halmashauri ndiko Madiwani mlipo, maendeleo ya kidorora hamuwezi kukwepa Lawama ni kama ambavyo Maendeleo ya nchini yakidhorota waheshimiwa wabunge hawawezi kukwepa kulaumiwa kwa sababu ndio wanaosimamia serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake, nilitaka hili mlitambue”.Alisema Kikwete.
Awali akitoa salamu za ukaribisho Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah amesema wanatambua heshima ya Halmashauri hiyo ambayo anatoka Rais wa awamu ya Nne hivyo kuimarisha umoja na ushirikiano katika kutekeleza mipango ya serikali.
“Tunatambua Heshima ya Halmashauri hii ambayo ametoka Rais Mstaafu awamu ya Nne tutaendelea kuilinda kwa Gharama yoyote ile, na mara zote nawaambia hawa ndugu zangu, tusifanye vitu kwa udogo kwasababu hapa kuna kiongozi mkubwa wa nchi hii ambae anaheshima ya kitaifa na kimataifa kwaiyo lazima tuwe madhubuti katika kupanga na kusimamia yote tunayokubaliana”. Alisema DC Zainab.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi amesema kwa mwaka huu wa fedha halmashauri hiyo imepanga kukusanya wastani wa shilingi Bilion 13.6 fedha ambazo zimepangwa kutumika kuboresha shughuli za maendeleo.
0 Comments