Header Ads Widget

CCM KIGOMA YATANGAZA MAJINA YA WANAOGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa kimetangaza majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwa chama na jumuia zake ambapo Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake na baadhi ya wenyeviti  wa Jumuia na  waliomaliza muda wao na kuomba kugombea tena majina yao yamekatwa.


Akitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Kigoma jana Katibu wa CCM mkoa Kigoma, Mobutu Malima alitangaza majina yaliyopitishwa na kamati kuu ya CCM kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali mkoani humo.


Katika nafasi ya Uenyekiti wa CCM mkoa waliopititishwa kugombea ni Pamoja na Jamali Tamim, Masoud Mtabiri na Joseph Masabo huku aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Amandus Nzamba alichukua fomu kugombea tena jina lake limekatwa.


Katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa waliopitishwa kugombea ni Abdulkadir Mushi, Salum Sasilo na Sahauri Kayandabila  huku mjumbe wa Halmashauri kuu anayemaliza muda wake akiteuliwa tena kugombea nafasi hiyo.


Aidha Malima aliwataja wanaogombea nafasi ya mwenyekiti wa Jumuia ya vijana (UVCCM) mkoa Kigoma kuwa ni Ngulungu Shaban, Emanuel Abuya, Felista Ntilampa na Jackson kalihamwe huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Geraidina Kabululu jina lake likikatwa.


Jumuia ya Wazazi waliopitishwa ni Nicholous Zakharia, Sakina Kabenza na Amosi Kidudu ambapo waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) mkoa Kigoma ni Agripina Buyogera na Anastazia Busungu huku Mwenyekiti anayemaliza muda wake jina likikatwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI