Header Ads Widget

TAKUKURU PWANI WANAOHARIBU MIRADI KUSHUGHULIKIWA

 


TAASISI ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Pwani  itawachukulia hatua baadhi ya watu wanaosimamia miradi ya maendeleo ambayo imeonekana kuwa na mapungufu.


Aidha Takukuru imefuatilia miradi 26 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.7 na kuikuta baadhi ikiwa na mapungufu.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Mkuu wa Takukuru mkoa wa Pwani Christopher Myava alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya kipindi cha robo mwaka Julai hadi Septemba.


Alisema kuwa uchunguzi unaendelea kwenye miradi hiyo na wahusika wakibainika watachukuliwa hatua kali.


Alitaja miradi iliyofuatiliwa kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, Barabara na Maendeleo ya jamii.


Alitaja mikakati waliyojowekea katika kipindi cha miezi mitatu ijayo kuwa ni kufanya ufuatiliaji na uchambuzi wa mifumo ili kuziba mianya ya rushwa itakayobainika.


Alibainisha kuwa bila rushwa maendeleo yatapatikana na huduma za jamii zitakuwa bora na zitapatikana kirahisi na kupunguza kero kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI