Na Hamida Ramadhani, Matukio daima AAP Dodoma
KATIKA kipindi cha mwaka 2020/2021,Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa elimu na usimamizi wa elimu (ADEM) umefanya tafiti mbalimbali zikiwemo za tathimini ya matokeo ya Mafunzo ya KKK kwa Walimu wa Darasa la III na IV yaliyofanyika Tanzania Bara.
Pia Wakala umefanya utekelezaji wa udhibiti ubora wa shule na utoaji wa mrejesho kwa walimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule za Msingi.
Haya yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa elimu (ADEM) Dkt Siston Mgullah wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya wakala huo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Alieleza Majukumu mengine ni kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wake, kuandaa na kusambaza makala na machapisho ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu.
“Wakala inaandaa mafunzo baada ya kufanya utafiti wa kujua mahitaji kwa wadau mbalimbali na malengo ya mafunzo hayo ni kuimarisha utendaji kazi katika ngazi zote za elimu kuanzia shuleni, katika kata, halmashauri, mkoa na wizara,”alisema .
Na kuongeza “Malengo mengine ni kuimarisha usimamizi wa utoaji wa elimu bora shuleni kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo ya elimu, kuziba ombwe la maarifa na ujuzi ambalo kiongozi au mtendaji hakupata katika mafunzo ya awali ya Ualimu na kuongeza idadi ya viongozi wenye maarifa ya uongozi na usimamizi wa elimu,”alisema Dkt Mgullah
Alisema Katika kipindi cha miaka mitano (2018- 2022), Wakala umetoa machapisho ya Moduli ya wajibu na majukumu ya Mjumbe wa Kamati na Bodi ya Shule,
Wajibu na majukumu ya Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Ualimu 2022
Alibainisha kuwa ,Moduli ya udhibiti ubora wa Shule wa ndani 2021 na uandaaji na usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule - 2018
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA ADEM KWA MWAKA 2021/2022
Aidha Wakala umedahili Walimu 1,839 katika mafunzo ya Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA) na Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule (DSQA) ili kuwapa ujuzi na maarifa walimu katika usimamizi, ufuatiliaji na tathmini katika elimu.
Alisema Wakala umetoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu udhibiti ubora wa shule wa ndani, kwa Maafisa 3,860 (REOs, RAOs, DEOs, WEOs) ili kuwajengea uwezo wa kusimamia ufundishaji na ujifunzaji wenye kuleta tija katika elimu.
Alisema Wakala umetoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu udhibiti ubora wa shule wa ndani kwa walimu 7,612 ili kuwajengea uwezo wa kusimamia ufundishaji na ujifunzaji katika shule wanazosimamia.
Wakala umeendesha mafunzo ya muda mfupi kwa Walimu Wakuu na Waratibu wa Taaluma 147 kutoka katika Shule za Msingi na Sekondari Zanzibar, chini ya mradi wa Mwanamke Initiative Foundation (MIF).
Alisema Wakala umeendesha mafunzo ya Kamati za Shule kwa Washiriki 126 katika Mkoa wa Songwe ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika Shule na umeandaa mtaala wa shahada ya menejimenti ya udhibiti ubora wa elimu ili kuimarisha usimamizi na utoaji wa elimu bora katika ngazi zote za elimu.
Alisema Wakala umefanya Tafiti sita na kuwasilishwa kwa wadau mbalimbali wa elimu ili kubaini mapungufu na kuandaa mafunzo wezeshi kwa wahusika,
Alisema Wakala umeandaa Moduli 3 katika eneo la Uongozi na Usimamizi wa Shule ili kuendesha mafunzo ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa ujenzi wa umahiri kwa walimu wa Shule za Sekondari Zanzibar na umeandika vitabu vya kujenga umahiri katika utekelezaji wa Mtaala wa Sekondari ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza kwa ajili ya Shule za Zanzibar.
MALENGO YA WAKALA KWA MWAKA 2022/2023
Alisema Kudahili Walimu 2343 katika Kozi za CELMA, DEMA na DSQA, kuandaa Kiongozi cha Mwalimu Mkuu na kuandaa Mwongozo wa Utawala Bora kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.
Alisema Imejipanga kutoa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Shule kwa Walimu Wakuu wapatao 17,000, kutoa mafunzo ya utawala Bora kwa wasimamizi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
0 Comments