Header Ads Widget

WAZABUNI WABABAISHAJI KUCHUKULIWA HATUA KALI NJOMBE DC

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


 Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang'anya ametishia kuwachukua hatua kali wazabuni wababaishaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo lake.


Nabalang'anya ametoa kauli hiyo katika  baraza la madiwani katika kikao Cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha wa 2022/2023 na  kwamba hayuko tayari kuwalea wazabuni wababaishaji katika kutekeleza kazi walizopewa na kwamba wakati wowote anatachukua hatua madhubuti kwa maslahi Mapana ya wananchi na taifa kwa ujumla.


Aidha amewaonya maofisa manunuzi wanaojihusisha na udanganyifu wakati wa ununuzi wa vifaa kwa kushirikiana na wazabuni hao na kwamba amewaomba madiwani kumuunga mkono pindi atakapochukua hatua dhidi ya wazabuni hao.



Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema baraza lake la madiwani lipo tayari kumuunga mkono mkurugenzi huyo pindi atakapochukua hatua hizo na kwamba kwa yeyote anayekwenda kinyume cha sheria hatoachwa salama.


Hongoli pia amewageukia watumishi wa halmashauri hiyo kuwa watakaotumia vibaya taaluma zao kwa kutaka kujinufaisha kupitia fedha ya umma nao hawawezi kusalimika kwani umakini mkubwa unahitajika katika ununuzi wa vifaa mbalimbali vya miradi ya serikali vyenye ubora.



Kwa upande wao baadhi ya madiwani akiwemo Innocent Gwivaha toka kata ya Matembwe na Roida Wandelage diwani viti maalum tarafa ya Makambako wamekiri kumuunga mkono mkurugenzi huyo kwani kumekuwapo kwa ubabaishaji mkubwa katika miradi mingi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI