Header Ads Widget

ACT YAJA NA USHAURI HUU KWA SERIKALI KUHUSU MAJI

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Chama Cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali kutoa ruzuku kwa mamlaka za maji mjini na vijijini ili kuwezesha kupanua na kuboresha miundombinu ya maji katika maeneo yao kwa kuzingatia mahitaji na usawa kwani maji ni huduma na sio biashara.


Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Sekta ya Maji na Mazingira Ester Thomas wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema bajeti ya wizara ya maji haiakisi mahitaji ya miradi iliyopo kutokana na miradi mingi kukwama kutokana na uhaba wa fedha. 


Aidha amesema hali ya upatikanaji wa maji Dar es Salaam umekuwa wa kusuasua hivyo Serikali iharakishe kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa bwawa la kidunda na mradi wa visima virefu 20 vya mpera na kimbiji pamoja na kushughulikia tatizo la upotevu wa maji linalotokana na uchakavu wa miundombinu.


Aidha, amesema ni vyema Serikali ikachukua mkopo nafuu wa muda mrefu wa shill trill 10 kutoka Benki ya Maendeleo ili kutekeleza miradi ya maji ambayo imeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha ili kuondoa adha ya maji kwa wananchi.


Amesema kuwa, changamoto iliyopo kwa sasa ya upatikanaji wa maji imesababishwa na Serikali kutokana na kueka mipango madhubuti ya kuweza kuisimamia Sekta ya maji kwani kuna vyanzo vingi vya maji nchini Tanzania havijatumika lakini kumekua na mgao wa maji unaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.


Aidha amesema, kwa upande wa mikoani changamoto ya upatikanaji wa maji inachangia sana watu wa maeneo ya vinijini kukumbwa na dimbwi la umasikini kutokana nakutumia gharama kubwa katika kupata maji.


" Ndugu wa waandishi wa habari mfano Kijiji Cha gehandu huko hanang mkoani Manyara mwananchi ananua maji pipa moja la lita 200 kwa shilingi elfu Saba, na familia moja inahitaji angalau pipa moja kwa matumizi yakujibana hivyo mwananchi huyu atahitaji shilingi milioni 2.5 Kwa  mwaka kwa ajili ya maji yakutumia yeye na familia yake" amesema Ester. 


Hata hivyo, amesema  kuwa Serikali inatakiwa kukamilisha miradi ya maji iliyokaa muda mrefu bila kukamilika na ile ambayo imeshindwa kutekelezwa kutokana uwepo wa ubadhilifu wa fedha za mradi huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI