Header Ads Widget

UVCCM YAWAKUMBUKA WALIMU WALIOTOA MCHANGO MKUBWA SHULE NYUMBU

 


KUTOKANA na kuona umuhimu wa elimu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kibaha Mjini Kata ya Mkuza imetoa vyeti na fedha kwa baadhi ya walimu wa masomo kwenye Shule ya Sekondari ya kutwa ya Nyumbu kwa kutoa mchango mkubwa kwenye ufundishaji.


UVCCM walitoa vyeti na fedha taslimu kwa walimu wa masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Baiolojia wakati wa mahafali ya 16 yayaliyofanyika shuleni hapo ambapo mgeni rasmi Kaimu Kamishna wa Elimu Bahati Chikwindo aliwakabidhi walimu hao.


Akizungumza juu ya utoaji wa zawadi hizo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mkuza Hashim Kibonge alisema kuwa walimu wa shule hiyo wameonyesha jitihada kubwa na kuifanya shule hiyo kuwa moja ya shule bora za kata kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha. 


Kibonge alisema kuwa wao kama vijana wameona wawape moyo wa kuendelea kufundisha kwa kujitoa ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri ambapo jitihada zao zimeonekana.


"Jitihada zao zimeonekana kwani kwa mwaka 2021 hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepata daraja sifuri na mwaka huu tunataka wapambane ili wapunguze daraja la nne na ikiwezekana kuliondoa kabisa,"alisema Kibonge.


Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkuza Matata Ngolo alisema kuwa wamekuwa wakiifuatilia shule hiyo na kuona jinsi inavyopambana kuhakikisha watoto wanapata elimu inayostahili.


Ngolo alisema shule hiyo licha ya kuwa na wanafunzi wengi lakini imeendelea kufanya vizuri kwenye Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambapo ufaulu kwa mwaka jana ilikuwa asilimia 99.


Kwa upande wake Naibu Kamishna huyo wa Elimu Bahati Chikwindo alisema kuwa ili wanafunzi waweze kufanya vizuri lazima pande zote zishirikiane baina ya wazazi na walimu.


Chikwindo alisema kuwa walimu wa Shule hiyo wanastahili pongezi kwani shule hiyo ndiyo shule inayoongoza katika mkoa wa Pwani kwa kuwa na wanafunzi wengi ikiwa na wanafunzi 2,136 na wanaotarajiwa kuhitimu ni 460.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI