Header Ads Widget

MKUU WA WILAYA NJOMBE AAGIZA KUKAMATWA YEYOTE ATAKAYEKWAMISHA UJENZI WA MADARASA

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Njombe na mkuu wa Wilaya ya Kissa Kasongwa amemuagiza mkuu wa polisi Makambako kuwaweka korokoroni wote watakaohusika kutaka kukwamisha ujenzi wa madarasa mapya yanayotarajiwa kuanza ujenzi wake sasa kwa ajili ya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi hapo mwakani.


Kasongwa ametoa agizo hilo akiwa katika shule ya sekondari ya mchepuo ya Mlumbe mjini Makambako mkoani Njombe ambapo amesema yeyote atakayecheza na fedha za ujenzi wa madarasa hayo hatoachwa salama.


Oman Diwani ni mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako ambaye anasema atatekeleza maelekezo ya kusimamia ujenzi huo kikamilifu.


Mkuu wa shule ya sekondari Makambako Godfrey Fwila pamoja na madiwani wa kata za Kivavi Alimwimike Sahwi na kata ya Lyamkena Salum Mlumbe wameahidi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kadri ya maelekezo ya serikali.


Halmshauri ya mji wa Makambako imepokea kiasi cha shilling milioni  420 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 21 katika shule 6 za sekondari.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI