Header Ads Widget

IEP YATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAM, MWANZA YAONGEZA


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Jopo la wataalamu wa elimu ya dini ya kiislam ( Islamic Education Panel) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika septemba 14,2022 ambapo jumla ya shule 3710 katika mikoa 25 na halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo huku shule ya Mumtaz iliyopo jijini  Mwanza imeibuka kidedea

Akizungumzia na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam,  wakati wa kutangaza matokeo hayo  Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Yusuph Kundecha, wakati akitangaza matokeo hayo amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani ni 142,522 sawa na asilimia 87.36 

Shekh Kundecha amesema kuwa  idadi ya watahimiwa ambao hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ni 20621 huku idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupataadaraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watahiniwa wote 142522 idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

"Watahiniwa na madaraja yao ni kama ifuatavyo waliopata daraja la kwanza (A) ni wanafunzi 3,567,daraja la pili (B) ni wanafunzi 22,587,daraja la tatu (C)ni 69,012,daraja la nne (D)45,781 huku.daraja la mwisho (E) ikiwa ni 15,575"amesema mjumbe huyo IEP 

Aidha, amezitaja shule 10 bora katika la shule zenye watahiniwa 20 na kuendelea,Sheikh  kuwa ni Mumtaz (Mwanza), Istiqaama(Tabora), Rahma (Dodoma), Algebra Islamic(Dar es salaam),  Dumila(Morogoro) Islamiya(Mwanza) Hedaru (Kilimanjaro), Daarul Arqaam(Dar es salaam), Mbagala Islami(Dar es salaam pamoja na Maarifa Islamic (Dar es salaam)

Hata hivyo, amesema kuwa shule 10 za mwisho zilizopata ufaulu mdogo kabisa ni pamoja na shule za msingi  Kilimani (Ilala), Mwasenga(Kigoma Ujiji), Umoja (Tabora), Bugoyi (Shinyanga), Mvuti(Dar es salaam) Kasamwa(Geita), Muzdalifa Islamic(Lindi), Mawala (Kilimanjaro) Sipungu (Tabora) pamoja na Izumangabo (Geita).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Education Panel Mohamed Kassim 

Pia alizitaja halmashauri 10 bora ni ambapo ikiongozwa na Hamashauri ya Wilaya ya Songea (Ruvuma), Mji wa Newala (Mtwara),Ngorogoro (Arusha),Ukerewe (Mwanza),Kalambo (Rukwa),Newala (Mtwara),Tunduma (Songwe),Mafia (Pwani), Mkuranga (Pwani) na Mji Nzega (Tabora).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI