Header Ads Widget

MCHUNGAJI MUNGE WA K.K.K.T -SONGEA AWATAKA WANANDOA KUACHA UBAGUZI.

 


Na Amon Mtega __Songea.

MCHUNGAJI Severi Munge wa Kanisa la Lutherani (K.K.K.T) Dayosisi ya Ruvuma amewataka wanandoa kuacha tabia ya kubagua ndugu wa mke au mume kwani kufanya hivyo kunachochea ndoa nyingi kuvunjika na kuifanya familia waliopewa na Mungu ibaki inahangaika kwa kukosa malezi.


 Munge ametoa wito huo wakati akihubiri kwenye ibada ya ndoa kati ya Tadei Njajule na Salome Sanga ambayo imefungwa katika Kanisa hilo liliopo Mjini Songea ambao wanandoa hao wanaishi Mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano mjini hapo.


 Mchungaji huyo amesema kuwa wanandoa wakishaanza kutengeneza matabaka ya ubaguzi wa kindugu kati ya mke na mume basi ni wazi ndoa hiyo inakuwamashakani kuendelea kustahimili.



 Amefafanua kuwa baadhi ya familia za wanandoa zimeharibika kimalezi kwa kutokuwa na maadili ni kutokana na Wazazi wao kutengana kwa sababu za matabaka ya kindugu.

 

Akihubiri kwa mifano amesema kuwa baadhi ya ndoa utakuta Wazazi wa upande wa kiume hawampendi mke wa kijana wao jambo ambalo hupelekea chuki na upande wa Wazazi wa kike kutokumpenda kijana wa kiume.



Aidha mchungaji huyo amewataka wanandoa ambao wapo tayari kwenye maisha waendelee kuvumiliana na kumuomba Mungu azidi kuwabariki licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali kwenye ulimwengu wa Dunia hii.

         

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI