Header Ads Widget

CBT, YAWATAADHARISHA WADAU WA KOROSHO KATIKA KUTOA TAARIFA

NA HADIJA OMARY MATUKIO DAIMAAPP LINDI 

WADAU  mbalimbali wa zao la korosho wameshauriwa kujiridhisha na usahihi wa taarifa kabla ya kuongea katika vyombo vya habari kuhusiana na zao hilo kwa madai kuwa zinapotolewa taarifa zisizo sahihi zinaleta taharuki na usumbufu usio wa lazima kwa wadau hususan wakulima.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya korosho nchini Francis Alfred wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi katika baadhi ya taarifa alizoziita ni za upotoshaji ambazo zimetolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ikiwemo bei za korosho,tozo zilizopo na suala la viuatilifu.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa bodi ya korosho Alfred amekanusha taarifa zilizosemwa kuwa viuatilifu vilivyosambazwa kwa msimu wa 2022/2023 vilikuwa feki Kwani vilihakikiwa mara tu baada ya kuingia Bandarini na kabla ya zoezi la usambazaji pia vilihakikiwa na taasisi ya udhibiti wa afya ya mimea na viuatilifu Tanzania na baadae kutolewa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi na Salama ya viuatilifu hivyo.

Kuhusu makato (tozo)zilizopo amesema jumla ya makato anayokatwa mkulima ni shilingi 205 kwa kilo na si 1113 Kama inavyosemwa na baadhi ya wanasiasa na kukanusha pia shilingi 81 zilizosemwa anakatwa mkulima kulipia deni la nyuma la magunia kwa kueleza kuwa wanunuzi hulipia shilingi 80..46 kulipia gunia ambalo akinunua korosho anaondoka nalo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI