Header Ads Widget

WAWEKEZAJI WAKARIBISHWA KUWEKEZA ZANZIBAR KATIKA KILIMO NA UFUGAJI

NA THABIT MADAI, MATUKIO DAIMAAPP,ZANZIBAR

MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema kuwa Serikali Mkoani humo ipo tayari kushirikiana na Makampuni Makubwa Duniani kuwekeza katika Kilimo na Ufugaji kwa lengo la kuleta tija kwa Vijana na Taifa kwa Ujumla.

Amesema Serikali tayari imeshafungua Milango kwa kuwakaribisha wawekezaji hao kutoka mataifa mbalimbali ili kuchochea Maendeleo ya Nchi.


Hayo ameyaeleza huko Mkoa wa Kusini Unguja wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya ziara maaulum ya kumtembelea Mwekezaji katika Kilimo cha Vanila na Vitunguu Swaumu ambapo ameeleza kuwa, Wawekezaji katika Sekta ya Kilimo wanachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi.



“Sisi kama Serikali tunawakaribisha wawekezaji mbalimbali hususani katika kilimo na Ufugaji ili vijana wetu waweze kupata ajira na kujikwamua na Umasikini sambamba na kuchangia ukuaji wa Uchumi wa Nchi yetu,”amesema.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi imejipambanua katika kuwakaribisha kuja kuwekeza Nchini katika Sekta mbalimbali.


“Naungana na Mhe Rais katika kuwakaribisha Wawekezaji, hivyo kwa upande wetu Mkoa wa Kusini Unguja tuna eneo kubwa ambalo linashauriwa Uwekezaji mkubwa katika shughuli za Kilimo na Ufugaji,” ameeleza.

Katika Maelezo yake ameonesha Kuridhishwa na maendeleo katika Mradi wa Vanila na kuahidi mashirikiano Makubwa na Mwekezaji huyo

 Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa Wito Kwa Wananchi mbalimbali kuacha tabia ya kuwadharau  Wawekezaji katika Maeneo yao huku akiwataka kushirikiana nao ili kukuza Miradi wanayowekeza na kuweza kupata faida kwa jamii.


“Mimi nataka kuwaambia na nipo tayari kutoa elimu kwa Wananchi kuwa tusiwadharau Wawekezaji badala yake tunatakiwa kushirikian nao ili kupata ajira katika miradi wanayowekeza,” amefafanua.

“Mfano Mzuri kwa Mwekezaji wa Vanila amekomboa Vijana wengi pamoja na kina mama ambao wamejikwamua kimaisha kupitia mwekezaji huyu,” ameongeza.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Vanila village Zanzibar Simon Mkodya ameeleza kuwa amerajika na kutembelewa na Mkuu huyo wa Mkoa huku akimuahidi kuendeleza Mashirikiano jamii katika utekelezaji wa Mradi huo.

“Siku ya leo kwangu ni bahati kubwa ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa ya Kusini Unguja ambapo ametembelea Mradi na kujionea hali halisi huku tukiahidi ushirikiano na Serikali ili kupata tija kwa Wananchi na Serikali,” amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI