NA HADIJA OMARY ,MATUKIO DAIMAAPP
VIONGOZI wa Dini wametakiwa kutowaaminisha wananchi juu ya tiba za kiimani ya uponyaji wa ugonjwa wa ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI) na badala yake wametakiwa kuwahamasisha wananchi ambao tayari wamegundulika na maradhi hayo kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo kwa usahihi.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa elimu ya Afya kwa Umma na mawasiliano (HPCO) Mkoa wa Lindi Bi, Habiba Chitanda wakati wa Mafunzo kwa viongozi wa dini Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuhamasisha upimaji wa vvu kwa jamii .
Chitanda alisema wapo baadhi ya wananchi ambao tayari wameshajigundua kuwa wanamaambukizi ya virusi vya ukimwa wanaokimbilia kwenye tiba za kiimani kwamba baada ya kuombewa wanapona hali inayowafanya baadhi yao kuacha kabisa kutumia dawa wanazopewa katika vituo vya kutolea huduma.
Alisema hali hiyo ni hatari kwa afya zao kwani kitendo cha kuacha kutumia dawa hizo kinawafanya virusi kurudi upya na kushambulia kinga mwili za mtumiaji kwa kasi Zaidi ya asilimia 100% ya awali.
Alisema viongozi wa kidini ni miongoni mwa watu mashughuli wanaoaminika katika jamii zetu hivyo wanao wajibu kukemea jambo hilo ili lisiendelee kufanyika na kuaminika na waumini wao.
Kwa upande wake mratibu wa kudhibiti virusi vya Ukimwi Mkoa wa Lindi. Dkt, Enock Chilumba alisema Tanzania ni kama Nchi nyingine duniani ipo katika mapambano ya kufikia 95% tatu za kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ifikapo 2030
Alisema 95 ya kwanza ni kuhakikisha watu wote wenye virusi vya ukimwi ambao hawafahamu hali zao wanafahamu 95 ya pili watu wote ambao watapima na kuonekana na virusi vya ukimwi waweze kuingia kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuanza dawa , 95 ya tatu ni kuhakikisha wale wote ambao wapo kwenye dawa , wanatumia dawa vizuri na atimaye waweze kufubaza virusi hivyo vya ukimwi.
Alisema hata mafunzo hayo waliyoyatoa kwa viongozi wa dini yanalenga katika kuhamasisha wananchi katika mabadiliko ya tabia na kuona umuhimu wa kujua Afya zao.
Naye Shekhe wa Mkoa wa Lindi, Mohamedi Mushangani aliisema kupitia mafunzo hayo ameweza kufahamu kuwa kinachopelekea wagonjwa wa VVU kupima na kuonekana kwamba hana virusi ni kutokana na utumiaji mzuri wa dawa za kufubaza virusi hivyo na sio kwamba vinatoweka kutokana na maombi ya shekhe ama mchungaji.
“kuzubaa kwa virusi haina maana kwamba wameondoka kabisa Hapana hivyo niwataadharishe waislam na wasio waislamu juu ya hawa wajanja wanaosema kwamba wanazo dawa za kuponyesha ukimwi sio kweli kwani ugonjwa huo sio lelemama ” alisema Shekhe mushangani.
Kwa upande wake Mkuu wa Jimbo katoliki KKKT Lindi (CCT) Woyzimen Simwanga alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kwamba ugonjwa huo wa ukimwi kwamba bado upo hivyo kila mmoja anapaswa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya na kuwa na utamaduni wa kuchunguza Afya zao mara kwa mara.
0 Comments