NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
Watu wenye ulemavu mkoani mkoani Kagera wameipongeza serikali kwa kuanzisha programu jumuhishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Tanzania inayolenga kusaidia watoto kuwa na utimilifu katika makuzi yao.
Hayo yamesemwa na makamu mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) halmashauri ya Bukoba, Filbert Bandihai katika mahojiano maalumu na chombo hiki baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa mradi huo iliyofanyika katika ukumbi wa ELCT uliopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
“Kupitia programu hii itasaidia wazazi katika mkoa huu kuwa karibu sana na watoto wao ili kufanya utambuzi wa watoto hao tangu wakiwa wachanga kama wanatatizo lolote, pia litakalosaidia watoto wenye ulemavu nao kujua haki zao za msingi kama vile haki ya kupata elimu ili na wao waweze kutimiza ndoto zao”
Aidha, amewaomba wasimamizi wa mradi huo kuzidi kutoa elimu kwa wazazi juu ya umuhimu wa malezi, makuzi na maeneo ya awali kwa watoto katika sehemu zote za mkoa huo sio kuishia maeneo ya mjini tu.
Naye meneja mradi mtandao wa malezi, makuzi na Maendeleo ya watoto wadogo Tanzania(TECDEN), Lazaro Ernest Tilito amesema kuwa, kuna muongozo ambao umeandaliwa na ofisi ya waziri mkuu unaolenga katika utambuzi wa awali kwa watoto wenye ulemavu ambao utasambazwa katika mikoa yote ilikusisitiza suala la utambuzi wa watoto tangu wakiwa watoto.
“kuna muongozo umeandaliwa na ofisi ya waziri mkuu ambao unaohusu watu wenye ulemavu utasambazwa mikoa yote lengo ni kufanya utambuzi wa awali wa watoto wenye ulemavu, nirahisi sana kumtambua mtoto kama anaulemavu endapo mlezi atakuwa na muhitikio wa kumuangalia mtoto kwa ukaribu ilihatua za kumsaidia mtoto huyo zifuate ” amesema Tilito.
Ameongeza kuwa mradi huu utatelezezwa kwa kipindi cha miaka mitano ukiwa na lengo la kudumisha makuzi, malezi na Maendeleo ya awali ya watoto chini.
Naye mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert John Chalamila ambaye alikuwa mgeni rasma katika uzinduzi wa mradi huo amewataka wazazi katika mkoa huo kuwa karibu na watoto wao ili kusaidia watoto wao kuwa na malezi na makuzi bora.
0 Comments