Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WALAANI MAUAJI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI LINDI

 

 


 

NA HADIJA OMARY _MATUKIODAIMA APP LINDI….



CHAMA cha ACT wazalendo kimelaani mauaji ya Wakulima na wafugaji ambayo yametokea katika baadhi ya maeneo Wilayani kilwa Mkoani Lindi , na kumtaka Waziri mkuu Kasimu Majaliwa kuwasimamia vyema mawaziri wenye dhamana kilimo ili wasiyaweke rehani Maisha ya wananchi wa maeneo hayo.


 

Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa chama hiko  cha ACT wazalendo Mkoa wa Lindi Isihaka Mchinjita alipokuwa anazungumza juu ya kifu cha Mkulimka Saidi Matimbanya alieuwawa kwa kuchomwa mikuki na wafugaji katika Kijiji cha kikole kata ya kikole Wilayani kilwa.


 

Katika taarifa yake mchinjita alisema kuwa marehemu Saidi Matimbanya alivamiwa na wafugaji shambani kwake siku ya tarehe 6/09/2022 majira ya saa nne asubuhi ambapo alikwenda shambani kwake akiambatana  na ndugu yake ndipo walipowakuta Ng’ombe Zaidi ya 100 wakichungwa na kula ndani ya shamba lake.

 

Mchinjita alieleza kuwa Ngombe hao walikuwa wanachungwa na kulishwa na akina mama wa kiimang’ati ambapo baada ya marehemu kuwahoji akina mama hao wafugaji ndipo ghafla wakatokea wafugaji wa kiume na kumshambulia na mkuki na kumuua.

 

Hata hivyo mchinjita alidai kuwa tukio hilo la mauwaji ya wakulima katika Wilaya hiyo ya kilwa  kwa Saidi Mtungunya sio la kwanza kutokea kwani yalishawahi kutokea Maeneo ya Nanjilinji, Nakiu na kikole ambako wafugaji wamekuwa wakiua wakulima na wakulima wamekuwa wakiua wafugaji

 

 

Kwa upande wake shuhuda wa tukio Msham Mohamed mkazi wa Kijiji cha kikole Wilayani Kilwa alisema kuwa siku ya tukio marehemu Saidi Mtungunya alikuwa kijijini kikole akiwa anaendelea na shughuli zake za kujitafutia kipato za ujenzi wa Nyumba ndipo akapokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Nanyati ambako marehemu alipokuwa anaishi juu ya wafugaji kuvamia katika shamba lake.


 

“baada ya kupokea taarifa hizo Saidi aliondoka moja kwa moja na kuelekea shambani kwake ndipo akawakuta wanawake wawili wakiwa na Ng’ombe wakiwalisha ndipo akaamua kuwaondoa wanawake wale pamoja na Ng’ombe wao”.


 

“ saidi akiwa anayafanya hayo alifyatua lisasi juu ili kuwatisha wafugaji hao wa kike waondoke ndipo walipotokea mwanaumje  mwingine kutoka vichakani ambae nae anadhaniwa kuwa ni  wafugaji akiwa na mkuki mkononi”.


 

“baada ya majibizano ya muda mchache kati ya saidi na Mfugaji yule wa kiume ndipo Saidi ambae ni marehemu aliamua kurusha risasi nyingine juu kumtisha mfugaji huyo ili aweze kuondoka kumbe lakini inaonekana baada ya kurusha risasi ganda la risasi halikutoka kwenye mashine”.


 

Mohamed lisema Saidi akiwa anahangaika kuondoa ganda la risasi kwenye bunduki yake ndipo mfugaji huyo akapata upenyo wa kuanza kumfukuaza saidi atimae akamfikia alipo na kuanza kumdhuru katika maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwemo tumboni na shingoni hadi kufaliki.

 

 

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji cha kikole Omary Atumani amekili kutokea kwa tukio hilo na mauaji ya Mkulima Saidi  Matimbanya yaliyotokea katika kitongoji cha Nanyati majira ya saa nne asubuhi.


 

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Wafugaji hao ni wavamizi ambao wanatokea katika vijiji vya Njinjo matole na zinga ambao wamekuwa wakiingia katika maeneo yao wakifuata Maji mto Matandu kwa ajili ya kunywesha mifugo yao ambao kwa mwaka huu wamekuwepo katika Kijiji hiko toka mwezi mai.


 

Bw. Athumani alisema kuwa licha ya Kijiji hiko kuwa katika mpango wa matumizi bora ya Aridhi ambayo akija tenga eneo la wafugaji lakini wafugaji hao wemekuwepo katika Kijiji hiko kwa miezi kadhaa sasa.


 

 

Hata hivyo Bw. Athumani alieleza kuwa Miongoni mwa jitihada zilizochukuliwa na uongozi wa Kijiji hiko ili kuwaondoa wafugaji hao ni kufikisha taarifa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ambapo aliwaita watendaji wa Halmashauri akiwepo na mkurugenzi kwa ajili ya kuwaondoa wafugaji hao toka mwezi wa sita mwaka huu.


 

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Eston Ngilangwa  alisema Katika kata ya kikole Kijiji kilichokubali kutenga eneo la wafugaji ni Kijiji cha Luhatwe huku Kijiji hiko cha kikole kikiwa na maeneo ya misitu ya hifadhi kilimo na makazi pekee.


 

Alisema jitihada zinazofanywa na ofisi yake ili kuwaondoa wafugaji hao hasa kwa wakati huu ambao wameanza kuleta madhara kwa wakulima ni kufanya msako ili kubaini eneo ambalo wamelivamia ambapo mpaka sasa baada ya tukio hilo la mauwaji kutokea tayari maofisa wa TFS , TAWA na Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Kilwa wapo katika Kijiji hiko kwa ajili ya zoezi hilo

 


Hata hivyo jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa huo wa Lindi ziligonga mwamba kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI