Header Ads Widget

SUALA LA TOZO BADO KIZUNGUMKUTI

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma


WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba amesema  suala la kodi ya tozo halita hairishwa kwani zoezi hilo limekuja kuunganisha nguvu kutekeleza mahitaji ya lazima ambayo yalikuwa pengine yanakosa bajeti.


Pia Serikali imewataka wananchi kuwa watulivu juu ya suala la tozo huku ikiwawashukuru wananchi hao kwa kutoa maoni yao  ya suala hilo la tozo na kwamba imewasikia, imepokea hivyo hivi karibuni itakuja na majibu sahihi.  


Akizungumza na waandishiwa habari  jijini Dodoma leo Septema 1, 2022 wakati akitoa ufafanuzi wa awali juu ya tozo Waziri huyo alisema serikali imeweka timu ya watu kwa ajili ya kuchambua tozo hizo  kwani ni lazima mtu alipe kulingana na kipato chake na sio kuwaonea wanyone huku wenye uwezo mkubwa wa kipato wakiachwa.


"Uhitaji wa bajeti kama nchi unaongezeka kwa sababu ya majukumu ya msingi kutokana na  miradi mikubwa  inayotekelezwa ikiwamo ya Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo bajeti yake ni Trilioni 6," alisema Waziri Nchemba


Alibainisha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki na za Jumuiya ya Kiuchumi nchi za kusini mwa Afrika (SADC), hakuna nchi inyotekeleza kwa mara moja miradi mikubwa kama Tanzania.


"Tanzania ina bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo  ni la lazima nchi inalihitaji tangu siku nyingi, bajeti yake ni zaidi ya Trilioni 6, Reli ya kisasa hadi kukamilika inahitaji zaidi ya trilioni 23,".


Na kuongeza“Kila Mtanzania anatakiwa ajisikie farahi kwa miradi mikubwa ambayo ni uti wa mgongo ambayo itageuza uchumi wa chi yetu, Chimbuko la tozo ilikuwa ni kwa ajili ya kuunganisha nguvu kama Watanzania ili tuweze kutekeleza mahitaji ya lazima ambayo yalikuwa pengine yanakosa bajeti. ,”amesema Waziri Nchemba.


Alisema walianza kama mapendekezo, serikali ikapendekeza wa wakilishi wa wananchi waliona hili jambo lina mantiki  walifanya kwa kuzingatia ulazima wa maeneo yenye uhitaji wa ulazima.


Waziri Nchemba aliyataja maeneo hayo kuwa ni madarasa, kujenga vituo vya afya, ununuzui wa vifaa, nyumba za walimu, ujenzi wa miundombinu huku akileza kuwa kabla ya mwaka mmoja uliopita ikilinganishwa na kule nyuma kuna tofauti kubwa barabara zilikuwa hazipitiki hata kidogo  lakini sasa zinapitia.


Amesema kuwa wanawekeza nguvu kwenye shughuli za kiuchumi  kwani vijana wengi hawana ajira  na wale wenye kipato kidogo wapo wengi hivyo serikali kupeleka nguvu kazi ya vijana hao waingie kazini huku akieleza kuwa kwa sasa wahitimu wanawategemea Wastaafu


Naye Waziri, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ameeleza kuwa tayari serikali imejenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi bilioni 117 na bilioni 149.5 zilitumika kwa ajili ya manunuzi ya vifaa kupitia tozo za mialamala ya simu.  


‘’Tozo hakika zimekuwa ni mwarobani katika kuboresha miundombinu pasipo kuwapo na vituo vya afya karibu kuna gharama kubwa kwa wananchi, naishukuru serikali kwa kuwezesha miamala ya tozo kupitia simu,’’ amesema Waziri Bashungwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI