Header Ads Widget

HILOLIMUS, TUACHE TABIA YA KUAGIZA GESI KWA NJIA YA SIMU

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMA APP MWANZA.


watumiaji wa gesi Mkoani Mwanza wametakiwa kuachana na tabia ya kuagiza gesi kwa njia ya simu badala yake wafike katika vituo husika ili kupata gesi iliyo na ujazo sahihi Kama inavyoonesha nje ya mtungi kwa kupima kwenye mzani.


Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja  Wakala wa Vipimo (WMA) Hilolimus Mahundi wakati akitoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi Bora ya mizani katika maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.


Mahundi amesema kuwa kuna ulazima wa kila mtu kuwa na uelewa juu ya ununuzi wa gesi na kuhakikisha wanafahamu matumizi sahihi ya mizani itakayosaidia kupunguza malalamiko gesi kuisha kabla ya wakati.


"Kumekuwa na shida kwenye matumizi ya gesi watu wanaagiza kwa kupiga simu, na wakati mwingine mtu anachukua bila kupima kwenye mzani anatumia ndani ya siku chache gesi inakata kumbe amechukua kwa kuangalia ujazo ulioandikwa kwa juu na kwa ndani ujazo huo haukufika" Alisema Mahundi.


Amesema kuwa Kumekuwa na baadhi ya wafanya biashara ambao sio waaminifu katika kazi zao kwa kuuza gesi ambayo Haina ujazo unaostahili na kupelekea kuwepo kwa changamoto katika matumizi ya gesi.


"Tuwashauri wananchi wanapokwenda kuchukua gesi wapime ili kuhakikisha kilichoandikwa juu kwenye mtungi ndicho kilicho ndani" Alisema Mahundi.


Kwa upande mwingine amefafanua kuwa Kumekuwa na baadhi ya wafanya biashara wa bidhaa za rejareja kutokuwa waaminifu katika mizani wanayotumia kwa kuchezea mawe wanayotumia katika kupimia bidhaa hizi.


"Wafanya biashara wamekuwa na mtindo wa kutelezesha mawe ya kupimia kwenye mizani, kwa mfano jiwe la kilo mbili limetelezeshwa Kumekuwa la kilo moja na nusu na mtu hawezi kujua" Alisema Mahundi.


Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanaponunua bidhaa yoyote Ile na kuona utofauti katika vipimo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI