Header Ads Widget

MWANAMKE AJIUA KWA KUSHINDHWA KUPATA TSH 30,000 YA MAREJESHO VICOBA

 


Suzana Sanga ambae ni Wifi wa marehemu Enea akizungumza na Matukio Daima 

MWANAMKE Mkazi wa Kihesa Kilolo B Kata ya Mkimbizi Katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa Enea Mkimbo (45) amejiua Kwa kujinyonga kukwepa usumbufu wa kudaiwa Tsh 30,000  marejesho ya wiki kwenye Vicoba .


Akizungumza na Matukio DaimaAPP Leo  mume wa marehemu Eneo ,Edward Sanga alisema kuwa mkeo alimuaga jana usiku kuwa anakwenda kusalimia ndugu eneo la Tumaini mjini Iringa.

Alisema kuwa mkeo hakuweza kurejea usiku na asubuhi wakati anajiandaa kwenda kazini ndipo alipobaini tukio la mkeo kujinyonga akiwa ndani ya chumba kilichokuwa kikitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu pamoja na Kuni .

"Kabla ya Kuondoka nilitaka kufunga mlango wa stoo ambao ulikuwa wazi na wakati nafunga niliona mke wangu akiwa amejinyonga Kwa kujifunga kamba juu ya paa la Nyumba " 

Kutokana na tukio hilo alilazimika kutoa taarifa Kwa Viongozi wa mtaa na ndugu kabla ya mwili huo kuchukuliwa na Polisi kupelekwa chumba Cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Hata hivyo alisema marehemu hakuwahi kumweleza kuwa anadaiwa zaidi ya kuona ujumbe kwenye simu yake ambao ulionesha chanzo Cha kifo chake ni kudaiwa marejesho ya shilingi 30,000 na wanakikundi wenzake .

Joram Gaitan ni kijana wa marehemu huyo alisema mama yake alikuwa akijishughulisha na shughuli za ujasiriamali na yeye hakuwa na taarifa ya mikopo hiyo japo Kwa upande wake hakuwa anaishi nyumbani hapo.

Akizungumza Kwa niaba ya marafiki wa marehemu Joyce Joseph  alisema chanzo Cha kujiua ni madeni ya vikoba aliyokuwa akidaiwa na kuwa siku moja kabla ya kujiua alionekana akizunguka mitaani kuomba kuazimwa pesa ya marejesho .

Joyce alisema kuwa kilichopelekea kujiua ni manyanyaso ya wenzake ambao walikuwa nao kwenye kikundi kumsumbua .

Wifi wa marehemu huyo Suzana Sanga alisema kabla ya wifi kuchukua uamuzi wa kujiua alifika nyumbani kwake kumweleza changamoto ya ulipaji wa deni Hilo ambalo deni lote lilikuwa ni Tsh Milioni 1 ambalo alikopa Kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ila Hadi Sasa alikuwa akidaiwa Tsh 300,000 ambazo Kila wiki marejesho yake ni Tsh 30,000 .

"Alikuja kuniomba nimuazime pesa nikamwambia sina ila achukue kitu chochote nyumbani kwangu akauze ama kuwekeza ili apate pesa ya kulipa marejesho ila aligoma na kusema hajisikii vizuri anaona kama ubongo umeganda vile Leo ndio nasikia kajinyonga  nimeumia Sana"

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuepuka kukimbilia kujiua pindi wanapokutana na changamoto mbali mbali bali washirikishe marafiki ama ndugu.

Post a Comment

1 Comments

  1. Kweli ukiwa na shida shirikisha wengine. Unaweza kuona ni shida kubwa kumbe kwa wengine ni ya kawaida tu.

    ReplyDelete



MAGAZETI



BBC NEWS