Header Ads Widget

DKT. MPANGO AAGIZA MRADI WA CHANZO CHA MAJI BUTIMBA UKAMILIKE DESEMBA MWAKA HUU.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Chanzo na Kituo cha tiba ya maji cha Butimba unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Ulaya ( EIB ) na Serikali ya Ufaransa ( AFD )  chini ya Mpango wa Uboreshaji wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa ziwa Victoria.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi  Antony Sanga amesema, mradi wa Ujenzi wa Chanzo na Kituo cha tiba ya maji Butimba unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya kiasi cha Shilingi Bilioni 69 ambao utakuwa na uwezo wa  kutoa lita za maji milioni 48 kwa siku,na kuhudumia wananchi wapatao laki moja na nusu.



Waziri wa Maji Jumaa Aweso,amesema Mradi wa Ujenzi wa Chanzo na Kituo cha tiba ya Maji cha Butimba, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa,Wakuu wa Wilaya pamoja na Wabunge wa Mkoa wa Mwanza watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili kero na adha ya maji iweze kuisha.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango ameiagiza Wizara ya Maji kusimamia Ujenzi wa Chanzo na Kituo cha tiba ya maji cha Butimba ili uweze kukamilika Desemba mwaka huu, ambao mkataba wake unapaswa ukamilke mwezi  Februari 2023.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS