Header Ads Widget

AJALI TENA MBEYA YAUA DED IGUNGA

Watu watatu wamefariki Dunia Katika ajali akiwemo mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Latu amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Inyala, Mbeya

Mbali ya mkurugenzi huyo pia dereva wa Lori na utingo wake wamefariki huku dereva wa mkurugenzi wa Igunga akijeruhiwa.
 
Ajali hiyo imetokea leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiwa anatoka kwenye kikao cha Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) jijini Mbeya.

Akizungumzia ajali hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Lucas Bugota amethibitisha kutokea kifo hicho.

Bugota amesema kuwa walikuwa wote kwenye safari lakini kwenye magari tofauti.

"Mi ndio naelekea huko kwani wao walikuwa nyuma yetu, yaani ndio hivyo tumepata msiba" amesema


Akizungumza na Matukio Daima Kwa njia ya simu Mweyekiti wa ALAT Taifa ambae ni mwenyekiti pia  Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Murshid Ngeze alisema kifo Cha mkurugenzi huyo kimemsikitisha na kuwa Mara baada ya kumaliza Kikao Cha ALAT Taifa kilichofanyika jijini Mbeya wakati Wajumbe wengine wakitembelea miradi yeye aliaga na kuanza safari ya kurejea Tabora .
 
 TAARIFA ZAIDI ITAKUJIA KUPITIA MATUKIO DAIMA HOTNEWS HIVI PUNDE  KUPITIA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS