Header Ads Widget

GUMZO LA USHINDI WA PS WA CCM MBINGA LATAWALA .

 




Na Amon Mtega, -Mbinga.


GUMZO la tawala Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma baada ya Katibu Muhutasi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani hapo  Raphaelis Nchimbi kushinda nafasi ya Ujumbe wa mkutano mkuu wa UWT Taifa  kwa kura 386 huku wapinzani wake Edisa Milinga kura 147 na Grance Quntine ambaye pia ni Mkurungenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji amepata kura 120 ambapo wapiga kura walikuwa 665.


Wakizungumza baadhi ya Wajumbe hao ambao hawakutaja majina yao baada ya uchaguzi huo wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa CCM  wamesema kuwa wamemchagua Katibu Muhutasi huyo kutokana na unyenyekevu wake kwenye Chama cha Mapinduzi katika utendaji kazi wake .


Wajumbe hao wamesema kuwa licha ya unyenyekevu wa mshindi huyo lakini wametuma salamu kuwa CCM ni Chama cha watu wote wanyonge na wasiowanyonge hivyo ni vema wakajenga tabia ya kuheshimiana ili Chama kiendelee kusongambele.


 Katika uchaguzi huo ambao nafasi mbalimbali zilipigiwa kura mgombea Grance Quntine alimuomba diwani wa Viti maalum Barubina Kapinga toka kata ya Nyoni aweze kumuombea kura kutokana na yeye kuomba ruhusa wa kutokuwa na nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.


 Nafasi hiyo ambayo ilionyesha kuwa na vituko vya aina kama ya mizengwe mgombea Raphaelis Nchimbi baada ya kujieleza alishangaa anapatiwa namba tatu badala ya namba mbili ambayo ilikuwa ni namba yake ambako ndiko jina lake lilivyokuwa likisomeka kwa wapiga kura tangu awali jambo ambalo lilimuibua msimamizi wa uchaguzi huo Saidi Nahoda kwa kutaka kanuni ya uchaguzi izingatiwe kila mmoja ambaye ni mgombea apatiwe namba yake halali na siyo vinginevyo.




Msimamizi Nahoda aliamuru kama kuna Wajumbe wameanza kupiga  kura zisimamishwe ili kila mjumbe awe na uhuru wakumchagua amtakaye jambo hilo lilifawanya Wapiga kura waibue shangwe za furaha za kumpongeza msimamizi huyo huku wakisema yupo imara ,ndipo katibu muhatasi alipoweza kushinda baada ya kupatiwa namba yake sahihi tofauti na awali ambapo alipatiwa namba tatu ambayo inadaiwa ilikuwa ni ya Grance Quntine .


Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu huyo Nchimbi amewashukuru Wajumbe kwa kumpatia nafasi hiyo na kuwa hatawaangusha pindi atakapofanya uwakilishi huo.

           

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI