Na MatukioDaimaAPP, Mbeya
Watanzania wametakiwa kulima mazao ya Mtama na Uwele kwakutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti zinazoweza kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza kwenye mahojiano na waandishi Mtafiti kutoka Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Homboro DK Joel Meliyo alisema kuwa kwa sasa tafiti za kina zinaendelea ili kupata mbegu bora zaidi ya mbegu zilizopo.
“Ukilima shamba la hekali moja unapaswa kupanda miche ya mitama elfu 18 ndio upate tani 3-3.8 mkulima anapaswa kupanda kwa mstari na aweke sentimita 30 na mtari na mstari 75 kila shina 10 unapata kilo moja na ukiweka pungufu lazima uzalishaji utashuka ushuka wakulima watembelee watalaamu ili kupata ushauri zaidi ambapo utasaidia uzalishaji kupanda na kulima kilimo chenye tija”
“Unajua mtama ni kilimo stahimilifu kwenye mvua kubwa na kidogo bado inastahimili ni zao ambalo linastawi sana lakini kwenye mvua chache linafanya viziuri zaidi watu wengi hawali mtama na hawalimi mtama ni vema wakajua faida na virutubishao lukuki vilivyopo kwenye mtama kuliko kwenye mahindi”
“Mtama unavirutubisho vya Zink , chuma na kopa madini ambayo sio mengi kwenye mahindi lakini kwa mtama umezidi pia una virutubisho ambavyo vinapunguza uzee mtama na ulezi, uwele vinanakuwa na nguvu zaidi kutokana na umeng’enywaji wake ni mdogo na unatoa sukari kidogo kidogo unasagwa polepole mwilini” alisema Dr Merio
MWISHO
0 Comments