Header Ads Widget

UMWAGILIAJI KUTUMIKA KUZALISHA MBEGU TARI ILONGA

 



Na MatukioDaimaAPP

Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania tari kituo cha ilonga inatarajia kuanza kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuzalisha mbegu za alizeti na mazao mengi kwa wingi  zaidi mkakati ambao utandana na kazi ya agenda 10/30. 


Akizungumza na matukio daimuapp Mkurugenzi wa  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Kituo cha Ilonga Morogoro Dr Emmanuel Chilagane alisema kuwa mikakati hiyo itakifanya kituo hicho kuongeza tija ya uzalishaji mazao bila kuangali kipindi cha msimu ama sio msimu. 


“Tunapanga kuwa miradi mbalimbali ya umwagiliaji ili kuweza kuzalisha mbegu kwakutumia umwagiliaji ili kupata mbegu” 


“Tunataka kufikia lengo la serikali la 2030 tuweze kuchangia pato la tatiifa na kufikia asilimia 10 kwa kilimo pekee”


“Kwa kupitia Maonyesho mbalimbali ambayo kwetu ni fursa kubwa kwa wakulima kujifunza teknolojia mbalimnbali huku watafiti wakipata fursa ya kufahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima vijijini hii kwetu inatupa hamasa ya kujua”


“Tunajipanga kutoa mbegu aina nyingi zaidi zenye tija kwasasa tunazo aina za alizeti ili kuwezesha wakulima walime kwa tija na kunufaika na tatifi ambazo tumekuwa tukifanya”


“Kituo chetu kina ratibu mazao ya alizeti, mikunde na mtama, ulezi na uwele na tunafanya tafiti za kuongeza thamani ili kuongeza tija kwa wakulima na walaji”


“Teknolojia zinazolenga mlaji ikijumuisha viwanda na pia kiasi cha viiini lishe ambavyo vipo kwenye mazao yetu ni muhimu sana ili kuboresha afya za watumiaji”


“Ukiacha uvumbuzi wa mbegu pia tunatoa mafunzo kwa wakulima kufahamu mbinu mbaliblai za kuandaa shamba, madawa ya kutumia  ili kuongeza tija kwenye mazao na kuhamasisha wakulima wajikite kwenye kilimo” alisema Dr Chilagane


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI