Na Amon Mtega, Mbinga
ZAIDI ya Wafanyakazi 150 wa mgodi wa Makaa ya mawe unaofanywa na kampuni ya TANCOAL katika eneo la Ngaka kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuingilia kati kutatua changamoto za mgodi huo ambapo hadi sasa unadaiwa umedorola kwenye uzalishaji.
Akizungumza mmoja wa Wafanyakazi hao Edson Bondi amesema kuwa hadi sasa hawajui hatima yao kutokana takribani zaidi ya miezi mitatu kutokuendelea na uzalishaji wa makaa hayo huku wafanyakazi hawajajulishwa lolote ya tatizo la mgodi huo.
Bondi amesema kuwa wao kama wafanyakazi wanaiomba Serikali iingilie kati ili kujua ni nini kinachokwamisha uzalishaji usiendelee kwenye mgodi huo licha ya makaa ya mawe bado yapo mengi na eneo ni kubwa.
Naye mfanyakazi mwingine Fredrick Nditi amesema kuwa inadaiwa awali waliambiwa kwa sasa kazi ya uchimbaji itafanywa na kampuni ya mirambo badala ya TANCOAL na kuwa mishahara watalipwa na Mirambo lakini wanashangaa kuona hakuna uzalishaji unaoendelea.
Kwa upande wake Mkurungenzi wa TANCOAL James Shedd akizungumza kwa njia ya simu kupitia mwanasheria wa TANCOAL Arafati Ssinare amesema kuwa nikweli kuhusu kusimama kwa mgodi huo miezi kadhaa na kuwa kuna taratibu zinaendelea kufanyika.
Afisa madini mkazi Mkoa wa Ruvuma Hamis Komando akizungumza kwa simu amesema taarifa za mgodi huo anazo na kuwa wenye mamlaka ni wenye mgodi na kuwa kazi ya Serikali ni kuhakikisha inapata kodi yake na siyo mambo mengine.
0 Comments