Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Kilimanjaro imewataka wafanyabiashara kuwasilisha kero mbalimbali wanazokumbana nazo kutokana na mfumo wa ulipaji Kodi kubadilika.
Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro Masawa Masatu amesema hayo wakati alipokuwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo wahasibu na wakaguzi na washauri wa Kodi kutokana na mabadiliko ya ulipaji wa Kodi nchi.
Amesema kuwa wako tayari kukaa na kushikiliza Kero za hao wafanyabiasha ili Kama kuna eneo litakalohitaji marekebisho waweze kulifanyia kazi.
"Tunataka kupata mrejesho kutoka kwenu namna tunavyofanya kazi na changamoto ambazo mnakabiliana nazo wakati sisi tunavyofanya kazi au maofisa wetu wanapofanya kazi huko ili mwisho wa siku tuweze kuwa pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu "Alisema Masatu.
Kwa upande wake Afisa msimamizi wa Kodi mkoa wa Kilimanjaro Oldupoi papa amesema kuwa seminar hiyo itawasaidia wahasibu na wakaguzi wa makapuni mbalimbali kijau Sheria na mabadiliko ya Kodi.
"Kwa hiyo kupitia mafunzo haya waahasibu au wataalaam hawa watapata kujua Sheria mbalimbali ambazo zimefanyiwa mabadiliko katika mwaka huu wa fedha"Alisema papa.
Ameendelea kusema kuwa wahasibu hao watapata elimu ya juu ya madiliko ya Kodi kupitia Sheria ya mwaka 2022 ilivyobadilika kwa baadhi ya maeneo na kusema Kuna maeneo ambayo Kodi imepungua na kwingine imeongezeka.
Hata hivyo amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wahasibu hao wametoa ahadi ya kwamba watatekeleza na kwamba watakuwa waamimifu kwa wafanyabiashara katika utekelezaji wa majukumu yao ili wafanyabiashara waasipate usumbufu wote kwa kutozwa adhabu na riba kutokana na kwenda kinyume na taratibu na Sheria za Kodi.
Kwa upande wa wahasibu walioshiriki katika seminar hiyo akiwemo John Maleo wameiomba serika itoe elimu hiyo kwa wingi hususani kupitia kwenye vyombo vya habari ili iweze kumfika Kila mmoja.
Wito wangu kwa Serikali ni kwamba mbali na mafunzo haya yanayotolewa kwa wadau wa walipa Kodi ,ni vyema ikarushwa kwenye vyomba vya habari Kama ilivyokuwa inafanyika katika kipindi Cha covid kwa sababu sio Kila mtu ana uwezo wa kuja kwenye semina na kwa kutumia vyombo vya habari itaasaidi kurahisisha utoaji wa elimu"Alisema Maleo.
0 Comments