Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Mkoa wa Njombe umetangaza kukamilisha zoezi la kuhesabu watu katika Dodoso kuu katika maeneo yote na kinachoendelea sasa ni zoezi la kuhesabu makazi kwenye sensa ya watu na makazi kwa mwaka huu.
Akitangaza kukamilika kwa zoezi hilo akiwa Tandala Ikonda Wilayani Makete mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema makarani na viongozi mbalimbali wameshirikiana vyema katika utekelezaji wa zoezi hilo na kwamba kinachoendelea sasa ni Dodoso la Makazi.
Awali mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda amesema wilaya yake imevuka lengo la makadirio ya uhesabuji watu katika kaya zao jambo ambalo limeonesha mafanikio makubwa ya sensa ya mwaka huu.
Akitoa taarifa ya ukamilishaji wa zoezi hilo Mratibu wa sensa wilaya ya Makete Bwana Aloyce Mwalukisa Amesema wamefikia asilimia 113 katika uhesabuji watu ndani ya wilaya yao.
Katibu tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary amepongeza hatua hiyo na kwamba jitihada za pamoja ndizo zilizofanikiwa zoezi hilo.
Baadhi ya wakazi wa Tandala makete akiwemo Evodia Mtweve,Boaz Mgenda na Pascaly Sanga wamekiri kufikiwa na makarani hao na kupewa ushirikiano wa kutosha katika maeneo yao.
Zoezi la sensa ya watu na makazi lilianza rasmi usiku wa kuamkia Agosti 23 na kutekelezwa katika kipindi cha siku Saba ambazo mkoa wa Njombe umeweka wazi ulipofikia
0 Comments