Header Ads Widget

TEMDO ARUSHA WABUNI MTAMBO WAKUCHAKATA MAFUTA YA ALIZETI

 

Na Pamela Mollel,Matukio DaimaAPP Arusha 

Taasisi ya Uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO)wabuni mtambo mpya wa kuchakata mafuta ya Alizeti yenye uwezo wakusafisha mafuta lita 1000 kwa siku


Akizungumza na vyombo vya habari katika maonyesho ya nane nane jijini Arusha,Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko Dkt Sigisbert Mmasi  alisema kuwa mtambo huo utakwenda kuwasaidia wajasiriamali kuboresha bidhaa zao ili kuendana na soko


Alisema kuwa mtambo huo wa kuchakata na kusafisha  mafuta ya alizeti ni kivutio kikubwa katika maonyesho hayo huku akitaka wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo 



"Awali kabla ya uwepo wa mashine hicho kulikuwepo na changamoto ya kusafisha mafuta hali iliyowalazimu wajasiriamali kuingia gharama kubwa kusafisha mafuta katika viwanda vikubwa"alisema Dkt Mmasi


Mbali na uwepo wa Teknolojia hiyo ya mashine ya kuchakata Alizeti pia TEMDO  wana mashine mbalimbali ikiwemo ya kutengeneza siagi ya karanga,mashine ya kuchakata unga lishe na viungo vya kupigia,mashine ya kuchakata zao la muhogo na sukari 


Pia wanatengeneza vifaa tiba kama vile vitanda vya kujifungia wamama wajawazito

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI