Header Ads Widget

VIJANA WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA KILIMO NA KUACHA KUSUBILI KUAJILIWA.

 


NA CHAUSIKU SAID, MatukioDaimaAPP

MWANZA.

Vijana ameshauriwa kuchangamkia fursa za kilimo na kuacha kusubili ajira kutoka  serikalini badala yake wafikilie namna ya kujikwamua kimaisha Ili wapige hatua kwa kilimo Cha mazao mbalimbali.


Hayo yamebainishwa na msemaji kutoka ofisi ya kilimo Manispaa ya Ilemela Karume Kanisius katika shamba darasa kwenye maonesho ya nanenae na kueleza kuwa kumekuwa na vijana wengi hawapendi kilimo na kutokiamini Hali inayopelekea  kuendelea kukaa mtaani bila kuwa na kazi yeyote na kujikuta wanaingia kwenye makundi yasiyofaa kwenye jamii.


Kanisius amesema kuwa vijana waweke Imani katika nyanja mbalimbali hususani katika kilimo kutokana na kuwa na fursa nyingi zatakazo wawezesha kujikomboa kimaisha.



"Vijana wengi hususani katika jamii yetu ya kitanzania hawakipendi kilimo na kutokiamini tuko hapa kwa watu wote hatujachagua lika hususani kwa watu wanaoamini ajira hazipo, na kuwa na mkingamo wa fikra hasi.

 

Ameeleza kuwa wanaendelea kuwatoa hofu na Imani waliyokuwa nayo tangu awali kwamba kilimo akifai wanahitaji kuajiliwa na watu waliopo kwenye kilimo wamesoma zaidi Yao. 



"tunawatoa wasiwasi, na vijana wanapotutembelea hapa tunawafundisha mbinu mbambali ambazo zitawasaidia kujikwamua kimaisha kulingana na mazingira anayotoka" Alisema Kanisius.


Kanisius ameeleza kuwa wamekuwa wakitoa ushauri kwa vijana kutokana na sehemu wanayoishi kulingana na ardhi Ili aweze kulima kilimo chenye manufaa na kuepukana na hasara Ili zisiweze kutoka.


Amesema kuwa vijana wakijitambua na kujiajili wenyewe katika sekta ya kilimo Kuna uwezo mkubwa wa kujikwamua kimaisha katika fursa ya kilimo


" Mtu yeyote yule ukiachana na vijana anayeingia katika kilimo huyo uwezi kumuajiri Tena mfano mwingine pia ni Mimi hapa nilienda kwa William lukuvi kufanya kazi nilishindwa kusubili hela ya kukadiliwa " Alisema Kanisius.


Aidha amewataka vijana na watu wenye lika tofauti tofauti kuondoa mawazo ya kuajiliwa na kukidharau kilimo,watafute mazingira mazuri ya kufanya kilimo hakuna atakayetaka kisubiri ajira, pamoja na kujifunza na kuachana na wazo ya kizamani kukaa nyunbani na kufikiria ajira badala yake

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI