Na Matukio DaimaAPP , Mtwara
Wakulima wa korosho zaidi ya laki moja nchini wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia teknolojia zilizofanyiwa Utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (Tari) ikiwemo namna ya kudhibiti magonjwa mbalimbali.
Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kusini katika mkoa wa Lindi mtafiti wa korosho kutoka Tari kituo cha Nalindele Hamida Bwaise alisema kuwa zao la korosho lina changamoto za wadudu na magonjwa kama ubwiliunga na bright.
"Tumejikita namna ya kudhibiti kwa namna ya asili ambapo akisafisha anapunguza vimelea vya magonjwa ama anaweza kutumia mbegu bora ambazo zimefanyiwa tafiti mbalimbali ambapo atapaswa kutumia viwatilifu kwa muda sahihi kiwango sahihi kwa maana kwamba mkulima anapaswsa kutembelea shmaba lake marakwa mara ambapo anaweza kutumia viwatilifu vya unga ama maji"
Akiona mashambulizi ya ubwiliunga anaweza kutumia kiwatilifu cha maji ama vya mfumo
Wadudu ama mbu wa mikorosho unapaswa kutumia viwatilifu vinavyoweza kuua wadudu hao
Wakulima wanapaswa kutembelea watalaamu ili wajifunze hatua ambayo itawezesha wao kujifunza na kuongeza tija kwenye mazao yetu
Mtafiti wa zao la korohso kutoka Tari Naliendele Kasiga Ndibanya
Pia kuepusha mikorosho kuambukizana magonjwa na wadudu pia ikikutana hushindwa kuzaa kwakuwa maua hudondoka
"
Shamba la korosho ukilianzisha lazima upogoleaji uwepo unakata matawi ya chini yote na kuwa kama mwamvuli ili matawi yote yanyaoelekea chini uyatoe na kuepusha na wadudu hata uokotaji wa korosho huwa rahisi zaidi "
Shamba jipya mkorosho ukiwa mdogo unashauriwa kupanda mazao ya msimu yenye soko karanga, kunde, ufuta ili kurudisha gharama zake za utunzaji wa mikurosho wakati akisubiri mkorosho kuanza kuvuna hii husaidia shamab kuwa safi na kuharibu mazalia ya wadudu na magonjwa
Dr Geraldina Mzena Mratibu wa zao la korosho kitaifa kutoka Tari Naliendele alisema kuwa ilu Mkulima apate faida anapaswa kufanya Kilimo biashara.
"Tunataka mkulima afanye kilimo bishara aangalie mbegu bora ambazo zinazaa korosho nyingi na kuzaa korosho bora kubwa na kuongeza tija kwa wakulima wa zao la korosho tunawafundisha waje kujifunza katika taasisi yetu"
"Korosho zinatakiwa kutunza vizuri kwakupogolea ili kudhibiti visumbufu vya mikorosho wadudu na magonjwa ili mikorosho ipate hewa na kutoa mazao yenye tija upuliziaji sahihi wa viwatilifu na tunaotoa elimu kwa wkulima ili wafuate kanuni za upuliziaji ambapo itasaidia wakulima kupata mazao mengi na yenye tija"
"Upuliziaji sahihi wa viwatilifu ambapo hufanya korosho zizae vizuri na zisishambuliwe na magonjwa"
"Ipo mikoa ambayo inakuwwa na changamoto ya mvua tunayoteknolojia ambayo inawezesha kukausha korosho kwa jua kidogo hususani wakulima wa mkoa wa pwani"
0 Comments