Na Matukio DaimaAPP,Mtwara
Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSC) kanda ya kusini imewataka wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuhakikisha kuwa wanatumia mbegu sahihi zilizodhibitishwa na taasisi hiyo.
Akizungunza wakati wa maonyesho ya nanenane kanda ya kusini Meneja wa Taasisi hiyo Dickson Rwabulala alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima ili kuweza kuzitambua mbegu sahihi zilizodhibitishwa na taasisi hiyo.
Kazi yetu kubwa ni kukagua na kufundisha na kusimamia biashara ya mbegu Tanzania kwa wanaohifadhi kuuza na kuzalisha mbegu nchini ambapo alisema kuwa endapo wakulima
Hapa tunachukua sampuli ili kuangalia uotaji na sampuli ya mbegu ambayo hupata lebo ya tosc kwenye pact ambapo tunashauri mkulima akinunua mbegu yoyote akwangue na kuingiza namba kwa kadri ya maelezo ambapo taarifa zikija tofauti anapaswa kutoa taaarifa kwenye mamlaka husika”
“Tunatoa elimu kwa wazalishaji wa miche ya matunda na mikorosho ili kuweza kuzuia magonjwa kueneo kwenye miti huwa pia tunafanya kaguzi huwa zinafanyika kwa kushtukiza sisi tunafahamuno za siri na stika huwa tunakagua mara kwa mara ili kubaini udanganyifu unaoweza kufanyika” alisema Rwabulala
Kwa upande wake Hamis Abdallah mkulima kutoka Wilayani Ruangwa alisema kuwa elimu hiyo ya kubaini mbegu kwakukwangua ameipata na ataifanyia kazi.
“Sisi huwa tunanunua mbegu hatujui zipi bora zipi sio bora ila zisipoota ndio tunaanza kutoa malalamiko kwa hizi taasisi nafikiri watafute namna ya kutufikia wawe wabunifu ili tuboreshe nchini” alisema Abdallah
MWISHO
0 Comments