Header Ads Widget

ALIYEMUONYA PADRI KITIMA SIKU CHACHE KABLA YA KUSHAMBULIWA AKAMATWA

 

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kumshikilia na kumuhoji, Dk Frey Edward Cosseny aliyemuonya kupitia mitandao ya kijamii, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima.

Dk Cosseny aliandika ujumbe wa kumuonya Padri Kitima na siku mbili baadaye akashambuliwa. Ujumbe huo aliutoa Aprili 28, 2025 usiku ukisomeka:

"Mwambieni Kitima iko siku ataingia kwenye 18 hatokaa asahau Tanzania muacheni ajifanye mwanasiasa. Mfikishieni message siku si nyingi atapata anachokitafuta dawa yake iko jikoni atakuja kuozea jela."

Kukamatwa kwake kumeripotiwa na Jeshi hilo, ikiwa siku chache zimepita baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa kuliagiza jeshi hilo kumtafuta na kumuhoji mtuhumiwa huyo aliyeandika kwenye mitandao ya kijamii siku za Kitima zinahesabika.

"Naliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta kwa haraka, yule mtu aliye-tweet kwenye mitandao ya kijamii kwamba, 'siku za Kitima zinahesabika'. Mtu huyu atafutwe haraka, ahojiwe ametumwa na nani, na hatua kali za kisheria zichukuliwe haraka iwezekanavyo, kwa watu wote watakaobainika kuhusika katika tukio hili," aliagiza Bashungwa, Mei 2, 2025.

Mtuhumiwa huyo anakuwa wa pili kutiwa mbaroni ikiwa siku tano zimepita tangu Padri Kitima kushambuliwa Aprili 30, 2025 kwenye makazi yake Kurasini jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya baraza hilo na hadi sasa amelazwa Hospitali ya Aga Khan akiendelea kupatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI