Header Ads Widget

TAKUKURU YAINGILIA KATI MGOGORO WA MWEKEZAJI (MAKOA FARM)NA CHAMA CHA USHIRIKA UDURU

 


Na Gift Mongi_Moshi


Hatimaye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoani Kilimanjaro imeanza uchunguzi dhidi ya mgogoro uliopo kati ya chama cha ushirika Uduru na mwekezaji wa Makoa Farm


Mgogoro huo ambao umeshadumu zaidi ya miezi sita Sasa ulipelekea uongozi wa chama hicho Cha ushirika kwenda shambani kwake ambalo ni mali ya chama hicho na kuweka makufuli ikiwa ni kumuamuru kuondoka.


Hatua hiyo ilitokana na kile kilichoeleza na mwenyekiti wa chama hicho Sael Mafuwe kuwa mwekezaji huyo alibadilisha matumizi ya ardhi Kama mkataba ulivyokuwa ukielekeza


"Tulikubaliana alime zao la kahawa lakini badala yake akageuza matumizi bila kutushirikisha sisi hivyo tukaamua kutumia njia stahiki katika kumuondoa"alisema


Mkuu wa taasisi hiyo mkoani Kilimanjaro Frida Wikes akizungumza na vyombo vya habari alisema tayari ofisi yake imeanza uchunguzi wa malalamiko yaliyowafikia za pande mbili yaani wenye shamba na mwekezaji aliyepo sasa. 


"Tumepokea malalamiko ya pande zote na tayari tumeanza uchunguzi maana wenye shamba la Makoa ni wanachama wa chama vha ushirika Uduru na mpangaji aliyepo sasa ambaye ni Makoa Farm"alisema 


Alisema malalamiko yaliyowasilishwa kutoka upande wa wamiliki hao ni kuwa mpangaji aliyepo sasa ambaye ni Makoa Farm (raia wa Ujerumani  Elizabeth Stegimaya)alibadilisha matumizi ya shamba hilo jambo ambalo ni kinyume cha mkataba unavyoelekeza.


Alisema makubaliano yaliyokuwepo ni kuendeleza zao la kahawa lakini matumizi ya ardhi yamebadilishwa na kwa sasa anaendesha shughuli za utalii ambazo ni kinyume na makubaliano waliyokubalina lakini pia shughuli hizo hazitoi nafasi za ajira kama ambavyo ni dira ya ushirika huo.


Kwa upande wake mwekezaji huyo Elizabeth Stegimaya naye alipeleka malalamiko katika taasisi hiyo akilalamika kuingiliwa katika shughuli zake licha ya kuwa alifuata taratibu zote za ubadilishaji wa matumizi ya ardhi na kuwa vielelezo vyote anavyo na pia alishirikisha uongozi wa chama cha ushirika lengo lake hilo. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI