Header Ads Widget

MZEE AFUMANIWA AKIBAKA MTOTO WA DARASA LA 6

 



 Mapuli Misalaba, Shinyanga


Mzee anayekadiriwa kuwa na umri wa Miaka 59 amefumaniwa na wananchi wa mtaa wa Masekelo katika Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa darasa la sita.


Mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo Bwana Elias Mminda amesema tukio hilo limetokea  Agasti 5, majira ya saa kumi na mbili jioni.


Mminda ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo ambapo amesema baada ya kufika katika eneo hilo alikuta wananchi wakimshambulia mtuhumiwa huyo.


“Majira ya saa kumi na mbili nilipigiwa simu nilikuwa nyumbani kwamba kuna bindi amebakwa lakini sasa ninataarifa naye toka siku nyingi kuwa huyu mzee anatabia za kuchezea wanafunzi baada ya kufika hapa nimekuta wananchi wamemkamata baadaye sasa nikawapigia polisi ndiyo wamekuja kumchukua”.


“Wananchi wamemkuta akiwa naye ndani nyumbani kwake maana huyu mzee anaishi peke yake tu wazazi wa mtoto wamesema walikuwa na taarifa toka siku nyingi kuwa huyo mtoto huwa anaenda kwa kwa huyo mzee na walikuwa wakitafuta mbinu za kumpata leo ndiyo wamefanikiwa lakini binti nimemuulizia amekili kuwa ni kweli huwa anakuja mara kwa mara kwa huyo mzee na amesema wameshafanya mapenzi mara nyingi tu”.amesema Mwenyekiti wa mtaa  Elias


Kwa upande wao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wakati wakizungumza  wameiomba serikali kupitia jeshi la Polisi linalohusika kulinda usalama wa raia kuwachukulia hatua watu hao wanaoharibu ndoto za wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI