Header Ads Widget

SERIKALI YASEMA ITAWALINDA WAWEKEZAJI

 



SERIKALI imesema itawalinda wawekezaji nchini kwa kutoruhusu bidhaa feki kuingia nchi. 


Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Liberata Mulamula wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa uzalishaji mbolea na viuatilifu hai katika kiwanda kiwanda cha kuzalishia bidhaa za kibiolojia Tanzania Biotech Products Limited.


Mulamula alisema kuwa serikali imeweka mikakati mahususi ya kuimarisha na kuendeleza sekta ya viwanda ili kuongeza ajira kwa wananchi ili kiwapunguzia umaskini.


"Tunaendelea kuwalinda wawekezaji wote wanaoamua kuanzisha viwanda hapa nchini kwa kuwapatia vivutio maalum ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara,"alisema Mulamula


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Exahud Kigahe alisema kuwa mkataba huo utatumika kutumia fursa ambazo hazijatumika na kiwanda hicho ni moja ya viwanda pekee Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.


Dk Grace Magembe mwenyekiti wa timu ya majadiliano ya Tanzania alisema kuwa timu kutoka Cuba na Tanzania na wataalamu zilikaa kwa siku 25 za majadiliano na kupitia hoja mbalimbali na mkataba ambao umehuishwa kwenye maeneo ya matumizi ya Teknolojia, mbolea na dawa za mazao ambayo haitumii kemikali.


Naye mkurugenzi mwendeshaji wa kiwanda hicho Nicolaus Shombe alisema kuwa watayafanyia kazi yote yaliyoko kwenye mkataba huo ili kuleta manufaa ya kiwanda hicho kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani.


Awali akikaribisha wageni mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa mkoa umeweka eneo kwa ajili ya uwekezaji ambako kuna kongani 23 za viwanda na matarajio ni kuwa na viwanda 350.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI