Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
IMEELEZWA kuwa kuanzishwa kwa wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)ni matokeo ya mabadiliko makubwa yaliofanywa na Serikali ili huduma ya maji vijijini kuongezeka, kuboreshwa na kuwa endelevu.
Akiongea na waandishi wa habari Mhandisi Mwajuma kondo walipotembelewa katika banda lao kwenye viwanja vya maonesho vilivyopo Nzuguni nanenane Jijini Dodoma alisema kuwa malengo ya RUWASA kwamuda mfupi ni kusimamia ujenzi wa miradi ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa Mazingira Vijijini yanafikiwa malengo ya asilimia 85 ifikapo Desemba 2023.
Alisema Mipango hiyo inahusisha na Kuendeleza ujenzi wa miradi 23 iliyo Katika hatua mbalimbali za utekekezaji kupitia fedha za mfuko wa Taifa wa maji (NWIF) na Bajeti ya mfuko Mkuu wa Serikali.
Aidha alisema lengo lingine la kuanzishwa kwa Ruwasa ni kuendelea utekekezaji wa mpango wa malipo (payment by results) ambapo katika mpango huo Kuna jumla ya miradi 50.
"Baadhi ya miradi inakarabatiwa na kupanuliwa na miradi mingine mipya iliyojengwa huku miradi 73 inaendelea kukamilika itaongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 794 ya sasa na kufikia asilimia 87.3 .
0 Comments