Header Ads Widget

RC NJOMBE ATANGAZA KUANZA CHANJO YA POLIO ..

 


Na Gabriel Kilamlya ,Matukio DaimaAPP Njombe 

Serikali mkoani Njombe imetangaza kuanza kwa kampeni ya chanjo ya polio awamu ya tatu kuanzia septemba 1 mwaka huu ikiwa lengo ni kuwafikia watoto 139,200.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema chanjo hiyo itasaidia kuwaepusha watoto na ugonjwa wa polio ambao hauna tiba zaidi ya kinga na itatolewa kwa muda wa siku nne.



Dokta Zabron Masatu ni mganga mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye anakiri kuwapo kwa ushirikiano mkubwa wa wazazi na walezi katika kampeni hiyo kwa awamu mbili zilizopita na kwamba anategemea kupata ushirikiano huo hata kwenye chanjo hii ya awamu ya tatu.


Mratibu wa chanjo mkoa wa Njombe Bi.Linda Chatila amesema ni muhimu kuwahisha watoto kupatiwa chanjo hiyo kabla hawajapatwa na polio.



Anna Augustino na Barani Makway  ni baadhi ya wazazi ambao wanasema hatua hiyo ya serikali itasaidia sana kuwasaidia watoto wao kuimarishwa kwa kinga za mwili.


Ugonjwa wa polio uliripotiwa katika nchi jirani ya Malawi kwa kisa kimoja jambo lililoilazimu serikali ya Tanzania kuanza kuchukua hatua za haraka kudhibiti ugonjwa huo kwa kuanza na mikoa jirani na nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI