Header Ads Widget

MGOMBEA UDIWANI IGWACHANYA NJOMBE ATAKIWA KUSAIDIA KUPATIKANA BARABARA ZA MITAA.

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mgombea Udiwani kata ya Igwachanya Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe kupitia Chama Cha mapinduzi CCM Evaristo Ng'ande(Makulumbi) ametakiwa kwenda kuhakikisha changamoto za kukosekana kwa barabara za mitaa na adha ya maji zinapatiwa ufumbuzi endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu. 

Wakizungumza mara baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Udiwani  kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi  ngazi ya kata wakazi hao akiwemo Andreas Mwalongo na Nuru Msemwa  wamesema wanatakani kuona kero hizo zinapatiwa majibu kupitia Mgombea huyo kwani adha ni kubwa.

Awali wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kata ya Igwachanya akiwemo Yohana Haule na Sara Nyagawa wamemtaka Mgombea huyo kwenda kuzingatia Sheria na kanuni zote katika zoezi la ujazaji Fomu na urejeshaji na hii ni kwa vyama vyote vya Siasa.

Mara baada ya kuchukua Fomu,Mgombea Udiwani kata ya Igwachanya Bwana Evaristo Ng'ande ametumia Fursa hiyo kuwashukuru wanachama na wajumbe wote waliomchagua kwenye kura za maoni  na kuahidi kwenda kuwatumikia endapo atachaguliwa.

Baadhi ya viongozi wa CCM kata ya Igwachanya na Mgombea Udiwani viti maalumu taarafa ya Mdandu Vumilia Kilamlya wamewaomba wanachama kuungana katika Kampeni ili kupata kura za kishindo za Chama hicho wakati ukifika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI