.
NA: FRANCO NKYANDWALE MATUKIO DAIMA APP SUMBAWANGA.
Mahudhurio ya wanafunzi wa Shule ya Msingi PITO yameongezeka kwa asilimia zaidi ya kumi baada ya kuanza kunywa uji shuleni hapo siku ya Jumatatu iliyopita.
Hayo yameelezwa na Mwalimu wa Taaluma Amos Malashi wa Shule ya Msingi PITO iliopo katika Halimashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani RUKWA kwenye kikao cha Kamati ya Shule Cha makabidhiano leo kati ya Mwalimu Franco Atubukeghe anayestaafu na Mwalimu Mkuu kwa sasa Abas Yussuf.
Mahudhurio ya wanafunzi yameongezeka kufikia asilimia 90 wiki hii tofauti na hapo awali ambapo mahudhurio yalikuwa ni asilimia kati ya 65 na 76 kuanzia darasa la Awali hadi la Saba mwaka huu ambapo Shule ina wanafunzi 637 na Walimu kumi.
Upatikanaji wa uji shuleni unatokana na wazazi kuchangia mahindi sado moja kutokana na kikao cha makubaliano cha wazazi cha tarehe 27 Juni, 2022.
Aidha Mwakilishi wa Afisa Elimu Kata ya PITO Mwalimu Benard Misika aliipongeza Kamati ya Shule kwa usimamizi na kuiomba Kamati hiyo kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la ulaji wa chakula shuleni kwani hutoa ufanisi mzuri wa kitaaluma kwa kuwa wanafunzi watakuwa na uhakika wa kula shuleni na kupunguza utoro.
0 Comments