Na Matukio Daima App Geneva, Uswisi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi, Mwenyekiti wa Jopo la WMO la kujenga uwezo wa Nchi Wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) "WMO Capacity Development Panel (CDP)", ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), ameshiriki na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya jopo hilo wakati wa Mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la WMO “Seventy-Fifth Session of the WMO Executive Council (EC-75)” uliofanyika katika Makao Makuu ya WMO, Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 20 hadi 24 Juni, 2022.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mikutano iliyotangulia ya WMO ambayo ni pamoja na Mkutano Mkuu wa 18 wa WMO "Seventeenth WMO Congress (Cg-18)" uliofanyika 2019, Mkutano Mkuu Maalum wa WMO wa 2021 (WMO Extraordinary Congress-2021) na mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la WMO.
"Seventy-Fourth Session of the WMO Executive Council (EC-74)" uliofanyika 2021.
Aidha, Mkutano huo wa 75 wa Baraza la WMO umetoa mapendekezo ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya hali ya hewa na maji yanayotakiwa kutolewa maamuzi na Mkutano Mkuu wa 19 wa WMO "Nineteenth WMO Congress (Cg-19)" utakaofanyika mwezi Mei, 2023.
Akiwasilisha ripoti ya jopo la WMO la kujenga uwezo "WMO Capacity Development Panel (CDP)", Dkt. Kijazi aliainisha mafanikio yaliyofikiwa kupitia kazi za Jopo hilo ambazo ni pamoja na hatua zilizofikiwa za mapitio ya miongozo ya mafunzo ya wataalamu wa hali ya hewa "Status of the review of Basic Instructional Packages (BIPs)".
Uundwaji wa chombo kitakacho waunganisha wadau wote wanaotoa elimu ya hali ya hewa na maji “Consortium of WMO Education and Training Partners (CONECT)” Mapitio ya mpango mkakati wa mafunzo wa WMO "Review the WMO Capacity Development Strategy (CDS)".
Maandalizi ya mwongozo wa kuhakikisha kuwa kazi za utoaji wa taarifa za hali ya hewa zinaendelea hata kipindi ambacho majanga kama UVIKO-19 yanapojitokeza, "Business Continuity and Contingency Planning Guidance".
0 Comments