Header Ads Widget

MAKINDA AWAOMBA WANANCHI KUTOA MAJIBU SAHIHI YA MASWALI YA SENSA

 


Na Mapuli Misalaba,MatukioDaima App  Shinyanga

Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi Tanzania Bara  Anne Makinda amewaomba wananchi kujibu ukweli wa maswali yatakayoulizwa kwenye zoezi la uandikishwaji wa Sensa ya watu na makazi ili kuirahisishia serikali kubaini mahitaji.


Ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema Sensa inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, Mwaka huu 2022 ni muhimu kwa watanzania wote.


Mheshimiwa Anne Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na makazi ili kufikia lengo lililokusudiwa na serikali katika kubaini mahitaji ya Taifa hilo.



Amewaomba wananchi hasa wasemaji wa kaya kutoa taarifa zenye idadi sahihi kwa karani atakayefika kuhoji kwani karani atakuwa na kiapo cha kutunza siri na iwapo atabainika kutoa siri atachukuliwa hatua za kisheria.


lengo la sensa siyo kujua wewe unamali kiasi gani lengo ni kujaribu kuona uzito wa uchumi wetu wa Nchi  uko namna gani kwahiyo watu waseme ukweli sensa haina jambo lingine lolote zaidi ya kupata changamoto zinazowagusa watu ilikusudi serikali  ije ijipange kutatua kwa usahihi hakikisha unahesabiwa mara moja lakini sema ukweli na hawa makarani wetu watakao kuja kukuhoji wanaapishwa kiapo cha kutunza siri za watu na iwapo atatoa siri zozote za mtu aliyekwenda kumhoji akijulikana tu anafungwa kwahiyo nawaomba wananchi wasiogope kutoa taarifa za mambo yao''. amesema Makinda


Aidha Makinda wakati akizungumza na wadau Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wananchi na utoaji elimu sahihi juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi amesisitiza uzalendo kwa kila mtu katika utoaji wa taarifa kwa makarani wa Sensa huku akiwaomba wadau hao kuendelea kutoa elimu hiyo kwenye maeneo ya watu zikiwemo taasisi za dini serikali pamoja na maeneo mengine ili wananchi waweze kujua umuhimu wa Sensa.


Kwa upande wake Mtakwimu kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) makao makuu bwana Pastory Ulimali  akieleza umuhimu wa Sensa amesema Sensa hiyo inakusanya taarifa ya kila kaya na siyo familia pekee na kwamba anayetakiwa kutoa taarifa ni mkuu wa kaya ambaye ni Baba au Mama.


Ulimani amesema taarifa za Sensa ya watu na makazi zitaisaidia serikali katika kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu pamoja na afya ambapo pia amesema taarifa hizo pia zitasaidia katika kutoa majibu ya msingi katika maswala ya kisiasa ikiwemo kutambua idadi ya wapiga kura.


Amesema mpaka sasa utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu katika Nchi nzima umeshakamilika ambapo amewaomba wadau kuwa mabalozi wazuri katika uhamasishaji na utoaji elimu kwenye jamii ili zoezi hili liweze kukamilika kwa asilimia mia moja.


 Baadhi ya wadau waliohudhuria katika kikao hicho wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa ushauri kwa serikali kuelekea sensa ya watu na makazi ambapo pamoja na mambo mengine wamepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na viongozi huku wakishauri kuwa viongozi kutumia Radio za kijamii ili kufikisha ujumbe kwa uharaka kwa wananchi walioko kijijini.


Naye Meneja Takwimu Mkoa wa Shinyanga Eliud Kamendu licha ya kupokea maoni na ushauri uliotolewa na baadhi ya wadau,ametumia nafasi hiyo kuomba vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa sensa ya watu na makazi ili kuondoa maswali kwa wananchi katika Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Nchini kote August 23,Mwaka huu.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI