Header Ads Widget

WAKULIMA NJOMBE WASHAURIWA KULIMA KILIMO CHA MSETO.

 


Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Wakulima mkoani Njombe wameshauriwa kujihusisha na kilimo mseto ili kujikwamua kiuchumi badala ya kutegemea zao la mahindi pekee.


Kauli Hiyo imetolewa na Aliyewahi kuwa  Mbunge  wa jimbo la Wanging'ombe Yono Stanley Kevella Mwaka 2005-2010 Katika uzinduzi wa albamu ya kwaya ya yerusalemu kanamalenga,ambapo amewataka wananchi hao kujihusisha na kilimo cha mazao tofauti  ikiwemo alizeti na parachichi badala ya kutegemea mahindi pekee.



Kevella amesema kilimo mseto kitawasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi hao kujikwamua kiuchumi,kwani hata pale ambapo zao moja bei inakuWa chini lakini zao lingine linakua na bei kubwa.


Baadhi ya wenyeviti wa serikali za vijiji wilayani Wanging'ombe akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kanamalenga Jafari Mkahala,Mwenyekiti wa kijiji cha mpululu Dickson Mdumba na Mwenyekiti wa kijiji cha Udonja Heri Mgute,Wamesema changamoto kubwa kwa sasa katika maeneo yao ni wanunuzi wa mazao kujipangia bei za kununulia mazao jambo ambalo linamuathiri mkulima.


Hata hivyo wananchi wa kijiji cha kanamalenga wamesema katika msimu wa kilimo ujao watahakikisha wanalima mazao tofauti ili kujikwamua kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI