Header Ads Widget

RC QUEEN SENDIGA AMUAGIZA DC IRINGA KUFUATILIA WAZEE OMBA OMBA KAMA WAPO KWENYE MPANGO WA TASAF

 


MKUU wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga amemuagiza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kufanya utafiti wa wazee wanaozunguka mitaani mjini Iringa kuona kama wapo kwenye mpango  kunusuru kaya masikini Tanzania (TASAF)na kama hawapo basi wawezwe kuingizwa kwenye mpango huo.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo mjini Mafinga wakati wa Kikao kazi Cha tathimini ya Kipindi cha Pili cha TASAF awamu ya tatu cha miaka minne kuanzia 2020 – 2023.

Sendiga alisema lengo la Serikali kutoa fedha za TASAF ni kusaidia walengwa wa mpango huo wakiwemo wazee hao ambao wanazunguka mitaani kuomba misaada hivyo kama wana sifa stahiki za kuingia kwenye mpango huo kuandikishwa ili waweze kunufaika .


Japo alisema kama wapo kwenye mpango huo wa TASAF na bado wanazunguka mitaani kuomba misaada si sawa kwani si lengo la mpango wa TASAF kusaidia watu wanaofanya shughuli za kuzunguka mitaani kuomba.



"Nimepata kuzunguka maeneo mbali mbali ya wilaya ya Mufindi na Kilolo nimeona jinsi mpango huu wa TASAF ulivyonufaisha walengwa kuwa na miradi ya kufanya ila Kwa Manispaa ya Iringa lazima uchunguzi ufanyike kama hawa wanaoomba mitaani ni wanufaika wa TASAF ama sio wanufaika"alihoji Sendiga 


Hata hivyo aliagiza watendaji wa mitaa na Viongozi wengine kutoka maofisini na kwenda Kwa walengwa ili kuendelea kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya fedha za TASAF Kwa kuzitumia fedha vizuri badala ya kutumia fedha hizo kunywea pombe .


Hata hivyo alisema mpango wa TASAF Ndani ya mkoa wa Iringa umekuwa na mafanikio makubwa Sana kutokana na walengwa kuwa na mafanikio makubwa ya kimaendeleo jambo ambalo linaonesha wazi mpango huo kuwa na faida .


Hivyo alisema iwapo wataalamu wa Kilimo na Mifugo wakatoka ofisini na kwenda Kwa walengwa kuwapa elimu ya Kilimo na ufugaji itasaidia walengwa wa TASAF kufanya shughuli zao kisasa zaidi .


Akitoa agizo kwa wakurugenzi wasio wajibika kushirikiana na waratibu wa  mpango huo wa TASAF alisema mpango huo unapaswa kusimamiwa na wakurugenzi wote bila kuwaachia waratibu pekee yao.


Kuhusu suala la ukatili wa kijinsia mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na kuendelea na Utekelezaji wa mpango huo wa TASAF mkoa wa Iringa unaendelea na mapambano ya ukatili wa kijinsia pamoja na tatizo la udumavu Kwa watoto .


Hivyo alitaka Kila mkazi wa Iringa lazima kuendelea na mapambano ya ukatili pamoja na lishe Kwa watoto huku wakihimizana kujiandaa na Sensa ya watu na makazi na kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 .


Awali washiriki wa Kikao hicho walieleza kusikitishwa na baadhi ya wakurugenzi kuuchukulia mpango wa TASAF kama ni mpango Yatima Kwa kutoa ushirikiano Kwa watalamu wa mradi wa TASAF.



Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dkt Abel Nyamahanga alisema suala la kuhakiki ombaomba wa mjini Iringa ni la msingi kwani litapunguza omba omba ambao ni walengwa wa mradi wa TASAF.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI