Header Ads Widget

UHOLANZI YAWEKEZA TRILIONI 2.4 TANZANIA

 


Mitaji yenye thamani ya zaidi ya Trilioni 2.4 imeekezwa nchini na makampuni kutoka Uholanzi.

 

Kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Uwekezaji (TIC), Uholanzi ni moja ya nchi kumi bora kwa uwekezaji nchini, ambapo miradi ya makampuni yake yenye jumla ya thamani ya dola Bilioni 1.063 imeweza kuajiri watanzania wapatao 15,000.


Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa TIC, Revocatus Rashel amesema hadi sasa kuna kampuni na miradi Zaidi ya 170 kutoka uholanzi iliyoandikishwa katika kituo cha uwekezaji na yote ikifanya vizuri katika ulipaji wa kodi za serikali.


Rashel alikuwa akizungumza katika mkutano maalum wa majadiliano baina ya wawekezaji kutoka uholanzi na taasisi za serikali uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Four Points jijini Arusha.



Balozi wa Uholanzi nchini, Wiebe de Boer, anasema kuwa kuna Zaidi ya makampuni 80 kutoka Uholanzi amabayo yamewekeza nchini Tanzania.


Makampuni hayo yamewekeza Zaidi kwenye viwanda vya mbegu za kilimo pamoja na shughuli za utalii.



“Ushirikiano baina ya Tanzania na Uholanzi una Zaidi ya Miaka 45 sasa,” aliongeza Balozi De Boer.


Kwa mujibu wa Balozi huyo wa Uholanzi, Shirika la Ndege la Uholanzi, yaani KLM imekuwa ikifanya safari za kila siku baina ya Amsterdam na Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa, kuonesha jinsi gani nchi hiyo inathamini sekta ya utalii na biashara Tanzania.



Akifunga rasmi mkutano huo, Mkurugenzi wa idara maendeleo ya uwekezaji, wizara uwekezaji, viwanda na biashara, Aristides Mbwasi, aliyemuwakilisha waziri wa uwekezaji viwanda na biashara, amesema kuwa majadiliano hayo yamewezesha wizara kupata mrejesho kutoka kwa wawekezaji kuhusu maendeleo ya biashara nchini.


“Hii itatusaidia kutatua changamoto zinazojitokeza na pia kupata mbinu ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini,” alisema Mbwasi.




Meneja wa Mamlaka ya Mapato, mkoani Arusha, Eva Magashi amesema kuwa TRA imefungua milango kwa ajili ya kupokea malalamiko na ushauri kutoka kwa wafanyabiashara nchini.


"Hii ni kwa sababu matatizo mengi yanayolalamikiwa hasa hutokana na kukatika kwa mawasiliano" alisema Eva

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI