Header Ads Widget

MBUNGE NDAKIDEMI AENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WA JIMBO LAKE.

 


Na WILLIUM PAUL.

WANANCHI wa kata za Kibosho Kirima, Kibosho kati na Kibosho magharibi katika Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wanatarajia kuondokana na changamoto ya kupata umeme mdogo (low voltage) baada ya Serikali kuyaingiza katika mradi wa kuimarisha greedi ya Taifa.




Akihoji swali kwa Waziri Nishati Bungeni, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi alisema kuwa kata za Kibosho Kirima, Kibosho kati na Kibosho magharibi katika jimbo hilo zinakabiliwa na tatizo la umeme mdogo.



"Je ni lini Serikali itasaidia kutatua changamoto ya kupatikana kwa umeme mdogo katika kata hizo kwani umeme huwa unawaka kuanzia saa tano usiku? " aliuliza Prof. Ndakidemi.



Akijibu swali hilo, Waziri wa Nishati, January Makamba alisema kuwa, ni kweli kabisa katika mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi mjini na Moshi vijijini kumekuwepo na changamoto ya kufifia kwa umeme na nguvu ndogo ya umeme.


Waziri Makamba alisema kuwa, Serikali imelibaini hilo na imeanza mradi mkubwa wa kuimarisha greed ya Taifa utakaosaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme ambapo maeneo yaliyoingizwa katika mpango huo zimo kata alizotaja Mbunge Prof. Ndakidemi.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI