Na Mwandishi wetu, Mtwara
Shirika la Realizing Education for Development (READ) Tanzania limekarabati jengo la maktaba katika shule ya Sekondari Mangamba kwa Ufadhili wa Wentworth Africa Foundation.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Read Tanzania Rebecca Liundi alisema kuwa wamefanikisha kukarabati jingo hili na kuweka vitabu 954 na thamani mbalimbali zikiwemo meza viti na shelfu, computer pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watoto na walimu ambapo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 33 za kitanzania.
Shule ilikuwa na uhitaji mkubwa wa maktaba wanafunzi hawakuwa nayo tunatambua kuwa wanamahitaji mengi lakini tumeanza na maktaba ambayo tunaamini kuwa itawasaidia kuongeza maarifa na uelewa miongoni mwa wanafunzi” alisema Liundi
Nae Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Mtwara Geofrey Kituye alisema kuwa shule hiyo imekuwa na nafasi kubwa ya kupata maktaba hiyo ambayo itasaidia wanafunzi hao kupata maarifa kwa njia ya vitabu.
Kitendo cha kuichagua shule hii ambayo ni miongoni mwa shule nyingi zilizopo katika mkoa huu ni jambo la kusimamia na kulitunza maadamu kinatusaidia kuongeza ufaulu na kuboresha elimu katika mkoa wetu tunawakaribisha
“Nimefurahi kumuona motto wa kidato cha kwanza akizungumza vizuri lugha ya kiingereza oneni wivu tumieni makata vizuri kila kitu unachokijua wewe hapa duniani kipo katika maandishi”
Nae Bakari Selemani mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Mangamba alisema kuwa uwepo wa maktaba hiyo umekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wote shuleni hapo.
“Unajua kitendo cha wadau kujitoa na kujenga maktaba katika shule yetu ni jambo kubwa ni shule chache katika manispaa yetu ambazo zina maktaba hii itatusaidia kwa kiasi kikubwa kujisomea na kuleta matokeo chanya”
0 Comments