Header Ads Widget

MKURUGENZI TARI KITUO CHA NALIENDE DRKT. FURTUNUS KAPINGA AWAPONGEZA WAGENI KUTOKA MOHELI NCHINI COMORO.

 


Na Mwandishi wetu, Mtwara


Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanznaia Tari Kituo cha Naliendele Dr Furtunus Kapinga amewapongeza wageni 18 kutoka katika kisiwa cha Moheli nchini Comoro waliofika kituoni hapo kujifunza . 


Akizungumza na ugeni huo alisema kituo hicho kimefika mbali katika tafiti ambapo kwa teknolojia walizonazo kituoni hapo zinakidhi soko la ndani na nje. 



“Tari tuko vizuri kwa teknolojia na Utafiti ambao una lenga kupata majibu ya mnyororo wa mzima wa thamani wa mazao husika mbegu bora jinsi ya kudhibiti wadudu wasumbufu  kwenye mavuno yanayopatikana tunaongeza thamani”


Mkurugenzi wa chemba ya wafanyabishara kutoka kisiwa cha moheli nchini Comoro Djabiri Mze Said  alisema kuwa ujio wa umelenga kutafuta fursa mbalimbali za kibiashara  na kujifunza.


“Tumeona uzalishaji mkubwa viwandani katika mkoa wa morogoro lakini pia tumefika mtwara tumeona tafiti mblimbali zinavyofanywa na watatafiti Tanzania sisi tumejifunza mengi na tumevutiwa sana kikubwa tunaona mabenki Tanznaia yawasaidie” alisema Said


Nae Mwabata wa ubalozi wa Tanzania nchini Comoro Halfani  Salem alisema kuwa ziara hiyo ilianzia Dar, Morogoro na Mtwara wakiwa na lengo la kukuza uhusiano wa kibishara na watanzania ambapo bidhaa nyingi zimekuwa zikichukuliwa kutoka Tanzania. 

Alisema kuwa zipo bidhaa nyingi zinachukuliwa huku na kwenda kuuzwa nchini Comoro kukuza uhusiano na kufungua fursa za kibiashara kati ya hizi nchi mbili.


“Tunaona changamoto kubwa ilikuwa ni namna gani tunaweza kuwasaidia wafanyabishara kuanza kuhifadhi fedha kwenye benki na kuja kufanya biashara” alisema Salem


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI