Header Ads Widget

WANANCHI TOENI TAARIFA ZA UKWELI KUHUSU UMILIKI WA MAJENGO-SETUMBI

  



Na Esther Machangu, IRINGA


Wananchi wametakiwa kutoa taarifa za ukweli zinazohusu umiliki wa majengo katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika agosti 23, 2022, ambapo katika zoezi hilo litaenda sambamba na Sensa ya Majengo.


Afisa Maendeleo ya Jamii mwandamizi kutoka wizara ya Ardhi Tumaini Setumbi aliyasema hayo Juni 22,2022 katika Semina ya siku mbili  kuwajengea uwezo Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Ili kuongeza uwelewa wa kutoa Habari zinazohusu Sensa ya mwaka 2022.



 "Sensa ya Majengo itatoa Takwimu za Majengo zitakazotumika kupatikana kwa taarifa za Makazi Nchini, na itahusisha Majengo yote ya Makazi,Makazi ya Biashara na Yale yasiyo ya Makazi,Alisema Setumbi.


Aidha aliongeza kuwa Sensa hii ya Makazi itasaidia  kuondoa Madhaifu yaliyojitokeza katika zoezi la Ukusanyaji wa Kodi kupitia Mita za Umeme.



"Changamoto zilijitokeza katika zoezi la Ukusanyaji wa Kodi za Majengo kupitia Mita za Umeme zitaisha kwani Mita ya Mwenye nyumba itajulikana hivyo Kodi ya Jengo itakatwa kwenye Mita yake pekee na kuondoa usumbufu kwa wapangaji" amesema Setumbi.


Semina hii ya Wahariri  51,kutoka  Vyombo mbalimbali vya Habari  imefanyika Mkoani Iringa katika Chuo Kikuu Kishiriki Mkwawa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI