MRADI wa Youth Agency Mufindi (YAM) na
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa waanza kutoa mafunzo ya kutengeneza pikipiki Kwa vijana 48 kutoka kwenye mazingira magumu ili kupunguza ukali wa Maisha .
Wakizungumza jana wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea Ukumbi wa Yatima Igoda Mufindi washiriki wa mafunzo hayo Anold Kalinga na Zedani Kabonge mbali ya kupongeza mradi wa YAM Kwa mafunzo hayo Bado wamesema mafunzo hayo ni mwanzo wa kuondokana na tatizo la ajira kwao .
Walisema kabla ya kuunganishwa na mradi huo wa YAM walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni na baadhi yao kushawishika kujiingiza Katika makundi hatarishi ya ulevi na mambo yasiyofaa.
Hivyo walisema kupitia mradi wa YAM na mafunzo wanayopatiwa ni wazi watakwenda kuwa tofauti na vijana wenzao na kuanzisha vijiwe vya kazi ya ufundi pikipiki vijijini kwao .
Huku mkufunzi wa mafunzo hayo Said Hassan akieleza mafanikio ya mafunzo hayo toka alipoanza kuwa vijana wameanza kuonesha mwanga wa kuwa mafundi .
Mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa Foxes Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland utakelekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi utanufaisha vijana na watoto wanaotoka katika familia duni zaidi ya vijana 770 atika vijiji 16.
0 Comments